UDSM KULETA MAPINDUZI BONGO MOVIE
Chuo kikuu cha Dar es Salaam siku ya alhamis tar 10 JAN 2013 imefanya exhibition ya movie yao ya kwanza iendayo kwa jina la CRUSH HUSUDA ambayo imechezwa kwa ushirikiano wanachuo toka Shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) na wale watokao Kitengo cha sanaa ama FINE AND PERFORMING ART (FPA) na baadhi ya mastaa toka bongo movie kama mzee Chilo.
Movie hiyo ambayo director wake ni Mwalimu wa chuo hicho Mr Issa Athuman Mbura inatarajiwa kuingia sokoni mwezi wa pili ambapo baadhi ya wadau walioiona siku hiyo wanadai wanaisubiri kwa hamu kubwa kuona wasomi wenye vipaji vipya ndani ya Bongo Movie wakifanya vitu vyao.
Mmoja wa watu waliokuwepo eneo hilo alikaririwa akisema '....though this is their first movie but a great change in the movie industry is experienced'
Movie hiyo imechezewa katika mazingira ya mkoa wa Dar es Salaam maeneo mbalimbali ikiwemo chuoni UDSM.
Mapinduzi haya yanonekana kutokuwa kwenye movie peke yake bali pia hata tamthilia ambapo kuna maandalizi juu ya tamthilia itakayokuwa ikienda kwa jina la MY CUMPAS ambayo pia muongozaji ni Mwalimu wao toka chuo hicho Mr Issa Athumani Mbura. Baadhi ya watu wamezungumzia kufurahishwa na na ujio huo wa tamthilia wakisema kuwa walizoea kuona tamthilia za vyuo vikuu vya nje katika Tv za nchi za huko kama vile Kenya
Kuona trailler click the link bellow
https://www.facebook.com/photo.php?v=3296570273249&set=o.224487574278753&type=2&theater
u did brilliant thing, thats hw the intellectual can change the society. big up my collides. am Mbasha from UDBS UDSM 2nd year. together ma meen. keepn on
ReplyDelete