Albert Chínụ̀á lụmọ̀gụ̀
Àchèbé mwandishi mkongwe barani afrika
,alizaliwa tarehe 16 Novemba
1930)
katika mji
wa Igbo kijiji cha Ogidi kilichopo
kusini mashaririki mwa nchini
hiyo, Ni
mwandishi wa vitabu mbalimbali Barani Afrika na dunia kwa ujumla
akitokea
nchi ya
Nigeria
Ameandika vitabu vingi vyenye riwaya, mashairi na insha, Hadithi zake zinazotumika
hadi sasa zinatumia mitindo ya fasihi simulizi ya lugha yake ya asili,
Kiigbo. Hata hivyo
ameandika hasa kwa
Kiingereza. Baadhi ya maandiko yake ni pamoja
Mwaka 1958, aliandika kitabu kilichovunja rekodi kwa kuuza nakala milioni
kumi sehemu mbalimbali ulimwenguni akakiita
"Things Fall Apart baadaye vikafuata
vitabu vingine lukuki vikiwemo
mwaka 1960, "No Longer At Ease’
mwaka1964, "Arrow of God"
mwaka 1973, "Girls at War")
·
(mwaka 1987, kwa Kiingereza
"Anthills of the Savannah")
Isaiah Okafo Achebe na Janet Anaenechi
Iloegbunam wazazi wa mwandishi huyu waliishi maisha maisha ya kitamaduni
yaliyokuwa na ukristo ndani yake ambayo yanatajwa kumsaidia motto wao Chinua
Achebe.
Baada ya mdogo
wake kuzaliwa ,familia yake ilihamia
katika mji wa Anambra sehemu ambako ndiko zilikokuwa
mila na tamaduni za kiigbo
Akiwa na umri mdogo mama yake pamoja na
dada yake Zinobia Uzoma walipenda
sana kumwadithia hadithi
mbalimbali zilizohusu maisha ya mila na\
tamaduni tamaduni zao
Mwaka
1936, Achebe alianza elimu yake
ya msingi katika shule ya kati ya St Philips' ambapo pamoja na kuwapo kwa maandamano wa kati huo ,
alitumia muda wake mwingi katika kupata elimu ya kidini
ambapo alionekana kuwa na uelewa mkubwa zaidi hali iliyomsaidia kupanda
kidarasa kwa haraka zaidi.
Chinua alipendwa sana na Walimu
wake ambapo mmoja aliweka
wazi kwamba ni mwanafunzi pekee
aliyekuwa na mwandiko mzuri darasani
pamoja ujuzi mkubwa wa kusoma
zaidi.
Pia alikuwa akihudhuria shule ya jumapili kila wiki
pamoja na huduma maalumu ya
kiinjilisti zilizokuwa ziktolewa
killa mwezi huku akiwa na mkoba wa baba yake
Akiwa na umri wa miaka kumi na mbili
Achebe aliondoka nyumbani kwao na
kuelekea katika kijiji cha Nekede
kilometer nne ukitokea mji wa owerri na kujiunga na shule ya kati ambayo kaka yake alikuwa
akifundisha.
Katika mji wa Nekede
alipata kutathimini mila na
tamaduni za kimbari ambao ulikuwa umejikita zaidi katika kuabudu miungu pamoja
na utoaji wa sadaka .
Mwaka 1944 muda ulifika kwa Achebe kubadili
shule ya sekondari ambapo alipewa mtihani na kufanikiwa
kujiunga
na
shule ya kifahari ya Dennis
Memorial Grammar School
iliyoko katika
mji wa Otisha pamoja na chuo cha serikali
kwenye mji wa
U muahia
Shule
hiyo ilianzoishwa na watawala ukoloni wa waingereza ambapo pia chuo hicho cha serikali
kilianzishwa 1929 kuwaelimisha wasomi wajao wa NIGERIA. Kiwango cha taaluma
kilikuwa ncha juu sana ,wanaume walipewa kipao mbele huku lugha iliyotumika
kufundishia ikiwa ni Kiingereza
Kutokana na uelewa mkubwa aliokuwa
nao katika shule hiyo ya sekondari ndani ya mwaka mmoja alisoma madarasa
mawili na hivyo kumfanya ahitimu kwa miaka mine, elimu ya sekondari badala ya
miaka mitano
Achebe
kwa wakati huo hakupendelea
sana michezo iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wenginebadala yake.
Alifanya upelelezi katika maktaba kubwa iliyokuwa shuleni hapo na kugundua
kupo kwa vitabu vya historia pamoja na riwaya mbali mbali ambazo alizisoma.
Mwaka 1948, katika maandalizi ya uhuru
wan chi ya Nigeria ,Chuo kikuu kipya kilianzishwa ambacho kwa sasa kinaitwa
Chuo kikuu Cha Ibadan, kwa wakati huo
kilishirikiana na Chuo Kikuu Cha London
Achebe alipata alama za juu katika
mtihani wa kujiunga na chuo hicho na kufanikiwa kupata nafasi ya kusoma bure katika chuo ambapo kwa mwaka
wa kwanza akapata msaada wa fedha
akisomea udaktari
Baada ya mwaka mmoja alibadili kozi hiyo ,nakuchukua masomo mengine ambayo ni Kiingereza ,Historia na theolojia
ambapo baada ya kubadili alipoteza nafasi ya kusomeshwa bure na alilazimika
kulipia masomo yake ya ziada
Baadaye serikali ilimpatia fedha
kidogo ambazo hazikutosheleza ambapo
pia chinua alilazimika kuchangisha
fedha katika familia yake na pia kwa
kaka yake aliyekuwa akifanya kazi serikalini alimchangia ili asikatishwe
masomo yake
Katika miaka , 1950 angali bado chuo
kikuu alianza kuandika
stori fupi ambapo story yake ya kwanza ilikuwa ni In a Village Church" ikijumuisha ya watu
waliko vijijini pamoja na taasisi za
dini ya kikristo Nyingine
zilizofuta "The Old Order in Conflict with the New" and "Dead Men's
Path" zikielezea vita kati utamadu na maisha ya usasa
Baada
ya kuwasili kwa professor Geoffrey Parrinder katika
chuo cha Ibadan kufundisha Ushirikiano wa kidini , Achebe alianza kupeleleza juu ya chimbuko la dini ya kikristo na
tamaduni za afrika.
Mwaka 1953, achebe alifanya mt ihani wake wa mwisho wa shahada yake ya kwanza katika chuo kiku
cha Ibadan na
kufaulu katika daraja la pili
ambpo alirejea nyumban kwao Ogidi kuoangalia machagu yake.
Baada
kuhitimu elimu yake alifundisha lugha ya kiingereza katika shule ya
biashaRA Oba AMBAPO 1954 akaanza
kufanya kazi na Shirika la utangazaji La
Nigeria NbC NA KUAHAMIA LAGOS. Alifanya
shughuli nyingi akiwa na shirika hili.
Katika vita vya Biafra 1967
iliyotaka kujitenn nga kwa jimbo
la Biafra Achebe aliunga mkono
vita hivyo ,alitumikia kama balozi wa watu wa taifa jipya la Biafra ,Baadaye serikali ilishinda NA Kuchukuwa
utawala wa jimbo hilo huku CHINUA kuwaombea msaada watu wa lililokuwa taifa lake.
Baada
ya utawala wa Nigeria kulichukuwa jimbo hilo 1970 aliamua kuwa mwanasiasa
lakini baadaye alijiuzulu kutokana kuwapo kwa mpasuko uliosababishwa na rushwa
kwa uliokuwa kwa wasomi wakati huo
Katika
miaka ya 1970 Chinua aliishi nchini Marekani kwa miaka mingi Ambapo 1990
alihamishia makazi ya kudumu nchini humo
baada ya kupata ajali ya gari iliyomsababishia ulemavu wa miguu
tangu
mwaka 2009 mpaka mauti ilipomkuta 2amekuwa
professa wa masomo ya kiafrika katika chuo kiku cha Brown kilichopo nchini Marekani