Uhuru ataka mashtaka yake ICC yafutwe
Uhuru
Kenyatta mahakamani ICC
Wanasheria
wa rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, wameiomba Mahakama ya Kimataifa ya
Makosa ya Jinai, ICC, kumfutia mashitaka yanayomkabili mbele ya mahakama hiyo.
Bwana
Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Taarifa zinazohusiana
Kikao
maalum cha mahakama hiyo kimefanyika wiki moja baada ya mashitaka dhidi ya
mshtakiwa-mwenza, Francis Muthaura, kutupiliwa mbali na mahakama ya ICC.
Mawakili
wa Kenyatta wanasema kuachiwa kwa Muthaura, pia kunafuta mashitaka dhidi ya
Kenyatta, lakini mwendesha mashitaka wa ICC amesema ana ushahidi zaidi dhidi ya
Uhuru Kenyatta.
Kesi
dhidi ya Bwana Kenyatta, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mapema
mwezi huu, na kutangazwa rais mteule baada ya kupata asilimia kidogo juu ya
50%, imepangwa kuanza kusikilizwa mwezi Julai.
Baada
ya matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka 2007 - wakati Bwana Raila Odinga
aliposhindwa dhidi ya Rais wa sasa Mwai Kibaki, zaidi ya watu 1,000 waliuawa na
wengine 600,000 kuachwa bila makaazi.
Bwana
Kenyatta, mtoto wa mwasisi wa taifa la Kenya, Jomo Kenyatta anatuhumiwa kupanga
mashambulio dhidi ya makundi ya kikabila yaliyokuwa yakimuunga mkono Bwana Odinga
kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.
Shahidi muhimu 'haaminiki'
Zaidi
ya Wakenya 1,000 waliuawa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Wiki iliyopita,
mwendesha mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda alisema kesi dhidi ya Bwana Muthaura
imetupiliwa mbali kufuatia baadhi ya mashahidi kuogopa kutoa ushahidi wao, huku
mwingien akikana sehemu ya ushahidi wake na kukiri kupokea rushwa.
Shahidi
muhimu - akijulikana kama shahidi namba nne - alikuwepo katika mkutano ambako
BwanaMuthaura na Bwana Kenyatta walituhumiwa kupanga kuwatumia kikundi cha
Mungiki kinachoogopewa nchini humo kuwashambulia Wakalenjin, ambao walionekana
kuwa wafuasi wa Bwana Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2007.
Kiongozi
wa mawakili wa Bwana Kenyatta, Stephen Kay anesema kwa kuwa shahidi namba nne
ndiye aliyemhusisha Kenyatta na kikundi cha Mungiki, kwa hiyo kujitoa kwake
katika ushahidi kuna maana kwamba Kenyatta hana kesi ya kujibu.
Uhuru
Kenyatta ashinda Urais Kenya
"kwa
kiasi fulani tumepoteza imani katika utoaji maamuzi kama tulivyotahadharisha
kikao cha kwanza cha mahakama cha kuthibitisha mashitaka, kutokana na aina ya
ushahidi uliokuwa ukitolewa , na tukapuuzwa," Bwana Kay tameiambia
mahakama ya ICC, ripoti kutoka shirika la AFP.
"Ushahidi
dhidi ya Bwana Muthaura ambao umelazimisha kuondolewa kwa mashitaka dhidi ya
Kenyatta ni sawa sawa na Bwana Kenyatta," amesema.
Amewaomba
majaji kurejesha kesi ya Bwana Kenyatta kwenye mahakama ya kuthibitisha kesi
ili majaji waweze kupitia ushahidi uliobakia kabla ya kuanza kesi kusikilizwa
na kuamua kama kuna ushahidi kamili unaothibitisha kesi hiyo kusikilizwa.
Mwandishi
wa BBC Anna Holligan kutoka The Hague anasema baada ya kufutwa kwa kesi dhidi
ya mtuhumiwa mwenzake, Francis Muthaura, kumekuwa na uvumi kwamba mashitaka
dhidi ya Bwana Kenyatta huenda pia ikatupiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment