Sunday, March 24, 2013

HUGO CHAVEZ............



HUGO CHAVES RAFAEL FRIAS
 
Iilikuwa ni  safari nyingine ya kuelekea miaka sita kwa kiongozi huyu wa Venezuela aliyedaiwa  kuwa misimamo isiyoterere

Rafiki wa wa watu  maskini ,pamoja na jitihada zake za kuikomboa nchi ya Venezuela ,kifikra na vilevile kiuchumi adui maradhi naye hakuwa mbali kwa kiongozi huyo.

Ugonjwa wa Saratani  uliendelea kuodhoofisha afya yake licha ya jitihada zilizofanywa kuutokomeza ugonjwa huo.

 Hugo Rafael Chavez Frias alizaliwa Julai 28, 1954. Alishika madaraka ya kuiongoza Venezuela tangu mwaka 1999.

Kufuatia itikadi yake ya kisiasa ya Kibolivarian na "Usoshalisti wa karne ya 21", alilenga katika kutekeleza mageuzi ya usoshalisti katika nchi kama sehemu ya mradi wa kijamii inayojulikana kama Mapinduzi ya Wabolivia, ambayo yameshuhudia utekelezaji mpya wa katiba, demokrasia shirikishi na kutaifisha viwanda kadhaa muhimu.

Hugo Rafael Chavez Alizaliwa Sabaneta, Barinas, akawa afisa kazi jeshini, na baada ya kutoridhika na mfumo wa siasa za Venezuela ambao aliuona kama wa rushwa na sio wakidemokrasia, alianzisha Vuguvugu la siri la Mapinduzi ya Kibolivarian-200 (MBR-200) katika miaka ya 1980 ili kuipindua serikali.



Baada ya tukio hilo ,serikali ya Rais Carlos Perez Andres aliamuru ukandamizaji mkali wa maandamano dhidi ya kupunguzwa matumizi,yaliongozwa na Chaves

Katika mapinduzi yaliyoshindwa dhidi ya serikali mwaka 1992, rais Chaves  aliishia kufungwa jela.

Alipotoka gerezani baada ya miaka miwili, alianzisha chama cha siasa, Fifth Republic Movement, na alichaguliwa kuwa rais wa Venezuela mwaka 1998.

 Hatimaye alipendekeza katiba mpya ambayo iliongeza haki kwa makundi yaliyotengwa na ilibadilisha utaratibu wa serikali ya Venezuela, hali iliyomfaya arudie tena madarakani  mwaka 2000.
 
Wakati wa muhula wake wa pili wa urais, alianzisha mfumo wa Misheni ya Kibolivarian, Halmashauri za Kijamii na vyama vya ushirika vinavyosimamiwa na wafanyakazi, wakati pia alitaifisha viwanda mbalimbali muhimu kwa maslahi ya taifa.

Wapinzani wakati huohuo, walionesha hofu kwamba alikuwa akiumomonyoa uwakilishi wa kidemokrasia na kujiongezea mamlaka, ambapo walijaribu kumwondoa madarakani kwa njia zote kupitia mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa mwaka 2002 na kura ya maoni ya mwaka 2003.
 

Alichaguliwa tena mwaka 2006, kufuatia kuanzisha chama kipya cha siasa, United Socialist Party of Venezuela (PSUV), mwaka 2007.

alijulikana kama mkosoaji wa ubepari na hasa uliberali wa kisasa, Chávez amekuwa mpinzani maarufu wa sera za kigeni za Marekani.

 Akifungamana mwenyewe na serikali ya ujamaa ya Fidel na kisha Raul Castrol ya Cuba, ya Evo Morales wa Bolivia, na ya Rafael Correa wa Ecuador.

Urais wake unaonekana kama sehemu ya “mrengo wa kushoto” ukiisafisha Amerika ya Kusini.

Amekuwa anaunga mkono ushirikiano wa Amerika Kusini na Caribbean na alikuwa mtu muhimu katika kuanzisha ushirikiano wa kanda nzima; Umoja wa Mataifa ya Amerika Kusini, Muungano wa Wabolivia kwa ajili ya Waamerika, Benki Kuu ya Kusini, na mtandao wa televisheni wa kikanda, TeleSur.

Ushawishi wake wa kisiasa katika Amerika ya Kusini ulimfanya jarida la Time kumuweka katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani katika miaka ya 2005 na 2006.



Hugo Chávez amefariki dunia  kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka hamsini na nne

No comments:

Post a Comment