Unapozungumzia suala sehemu binadamu kuwepo kitu cha kwanza
kuangalia ni suala la usalama kasha mambo mengine hufuata
Binadamu
anahitaji kuwa salama na ndio maana mtu yeyote anapotaka kutembelea mahali
popote kitu cha kwanza kuulizia ni suala la usalama awe mwenye mtanzania au mtu mgeni toka nje ya Tanzania
Kwa
wiki hii tunaangazia eneo la kupumzika hapa Dar es Salaam liitwalo Mikadi Beach
lipatikanalo Kigamboni
Hii ni beach iliyojihakikishia usalama wa hali ya juu na
huduma mbali mbali za kibinadamu kwa umakini wa hali ya juu
Akizungumza
na NIHABARISHE meneja wa Mikadi beach bwana Fransis Raphael amesema kuwa beach
hiyo imejitosheleza kila kitu kwa malazi chakula na starehe za aina mbalimbali
kama kuogelea na burudani mbalimbali
‘’Suala
la usalama wa mtu ni muhimu sana na ndio maana sisi tuna ulinzi wa kiteknolojia
na wa binadamu manake mteja akiwa hapa na kupata tatizo hawezi kuja tena na
hawezi kufahia kuwepo hapa, tunapokea wageni wa aina mbalimbali na ndio maana
wafanyakazi wetu ni wa kutoka nchi mbalimbali’’
Mikadi tangu kuanzishwa kwake na kuchukuliwa na
wamiliki wa sasa mwaka 2008 pamekuwa na kimbilio la watu wa aina mbalimbali
tokana na huduma zake
Kwa
mujibu wa Bwana Francis Raphael Mikadi inaweza kuhudumia zaidi ya watu 150 kwa
siku moja.
Mikadi imekuwa
ni eneo ambalo watu mbalimbali toka ndani na nje ya nchi hufanya harusi zao na
kupata huduma safi
Kutokana
na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia Mikadi nao hawako nyuma kutokana
na kuboresha huduma za kuwasiliana na wateja wao kisasa zaidi kupitia mtandao
ambao wa www.mikadibeach.com ambao upo tayari
kila wakati kubadilishana mawazo na watu wahitajio huduma mahali pale
No comments:
Post a Comment