Saturday, March 23, 2013

PROF. CHINUA ACHEBE AAGA DUNIA

 
Albert Chínụ̀á  lụmọ̀gụ̀ Àchèbé  mwandishi mkongwe barani afrika ,alizaliwa  tarehe  16 Novemba 1930) katika mji wa Igbo  kijiji cha  Ogidi  kilichopo kusini mashaririki mwa nchini  hiyo, Ni mwandishi wa vitabu mbalimbali Barani Afrika na dunia kwa ujumla  akitokea  nchi ya Nigeria
Ameandika vitabu vingi vyenye riwaya, mashairi na insha, Hadithi zake zinazotumika hadi sasa zinatumia mitindo ya fasihi simulizi ya lugha yake ya asili, Kiigbo. Hata hivyo ameandika hasa kwa Kiingereza. Baadhi ya maandiko yake ni pamoja
Mwaka 1958, aliandika kitabu kilichovunja rekodi kwa kuuza nakala milioni kumi sehemu mbalimbali ulimwenguni akakiita  "Things Fall Apart baadaye vikafuata vitabu vingine lukuki vikiwemo
mwaka 1960, "No Longer At Ease’
mwaka1964,  "Arrow of God"
mwaka 1973,  "Girls at War")
·         Shida na Nigeria (mwaka 1984, kwa Kiingereza "The Trouble with Nigeria")
·         (mwaka 1987, kwa Kiingereza "Anthills of the Savannah")
·         Picha ya Afrika (mwaka 2000, kwa Kijerumani "Ein Bild von Afrika")
 Isaiah Okafo Achebe na Janet Anaenechi Iloegbunam  wazazi wa mwandishi huyu  waliishi maisha maisha ya kitamaduni yaliyokuwa na ukristo ndani yake ambayo yanatajwa kumsaidia motto wao Chinua Achebe.
Baada ya  mdogo wake kuzaliwa ,familia yake  ilihamia katika mji wa Anambra sehemu ambako ndiko zilikokuwa  mila na tamaduni za kiigbo
Akiwa na umri mdogo mama yake pamoja na dada yake  Zinobia Uzoma  walipenda  sana kumwadithia  hadithi mbalimbali zilizohusu maisha ya mila na\  tamaduni tamaduni zao
Mwaka  1936, Achebe  alianza elimu yake ya msingi  katika shule ya kati ya  St Philips' ambapo  pamoja na kuwapo kwa maandamano wa kati huo , alitumia  muda wake mwingi  katika kupata elimu  ya kidini  ambapo alionekana kuwa na uelewa mkubwa zaidi hali iliyomsaidia kupanda kidarasa kwa haraka zaidi.
Chinua alipendwa sana na Walimu wake  ambapo mmoja   aliweka  wazi kwamba  ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na mwandiko mzuri darasani  pamoja  ujuzi mkubwa wa kusoma zaidi.
   Pia  alikuwa akihudhuria  shule ya jumapili  kila  wiki  pamoja na huduma maalumu ya  kiinjilisti  zilizokuwa ziktolewa killa mwezi huku akiwa na mkoba wa baba yake
Akiwa na umri wa miaka kumi na mbili Achebe  aliondoka nyumbani kwao na kuelekea katika kijiji cha  Nekede kilometer nne ukitokea mji wa owerri na kujiunga  na shule ya kati ambayo kaka yake alikuwa akifundisha.
Katika mji wa  Nekede  alipata kutathimini  mila na tamaduni za kimbari ambao ulikuwa umejikita zaidi katika kuabudu miungu pamoja na utoaji wa sadaka .
Mwaka 1944 muda ulifika kwa Achebe kubadili shule ya sekondari ambapo alipewa mtihani na kufanikiwa  kujiunga  na  shule ya kifahari ya Dennis Memorial Grammar School  iliyoko katika mji wa Otisha pamoja na chuo cha serikali  kwenye mji wa U muahia  
Shule  hiyo ilianzoishwa na watawala ukoloni wa waingereza  ambapo pia chuo hicho cha serikali kilianzishwa 1929 kuwaelimisha wasomi wajao wa NIGERIA. Kiwango cha taaluma kilikuwa ncha juu sana ,wanaume walipewa kipao mbele huku lugha iliyotumika kufundishia ikiwa ni Kiingereza
Kutokana na uelewa mkubwa aliokuwa nao   katika shule  hiyo ya sekondari  ndani ya mwaka mmoja alisoma madarasa mawili  na hivyo kumfanya ahitimu  kwa miaka mine, elimu ya sekondari badala ya miaka mitano
Achebe  kwa wakati huo hakupendelea sana michezo iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wenginebadala yake.
Alifanya upelelezi katika maktaba kubwa iliyokuwa shuleni hapo na kugundua kupo kwa vitabu vya historia pamoja na riwaya mbali mbali ambazo alizisoma.
Mwaka 1948, katika maandalizi ya uhuru wan chi ya Nigeria ,Chuo kikuu kipya kilianzishwa ambacho kwa sasa kinaitwa Chuo kikuu Cha Ibadan,  kwa wakati huo kilishirikiana  na Chuo Kikuu Cha London
Achebe alipata alama za juu katika mtihani wa kujiunga na chuo hicho na kufanikiwa kupata nafasi  ya kusoma bure katika chuo ambapo kwa mwaka wa kwanza akapata msaada wa fedha  akisomea udaktari
Baada ya mwaka mmoja  alibadili kozi hiyo ,nakuchukua  masomo mengine  ambayo ni Kiingereza ,Historia na theolojia ambapo baada ya kubadili alipoteza nafasi ya kusomeshwa bure na alilazimika kulipia masomo yake ya ziada
Baadaye serikali ilimpatia fedha kidogo  ambazo hazikutosheleza ambapo pia   chinua alilazimika kuchangisha fedha katika familia yake na pia kwa  kaka yake aliyekuwa akifanya kazi serikalini alimchangia ili asikatishwe masomo yake
Chuo kikuu kipya cha Ibadan  kilikuwa na kitivo makini cha Lugha  ya Kingereza   pamoja na  waathiri mashuhuri ambao pia ni waandishi wa vitabu  ka vile Nobel Laureate Wole Soyinka,,Elechi Amadi, John Pepper Clark na Christopher Okigbo.[26]
Katika miaka , 1950 angali bado chuo kikuu  alianza  kuandika   stori fupi ambapo story yake ya kwanza ilikuwa ni  In a Village Church" ikijumuisha    ya  watu waliko vijijini  pamoja na taasisi za dini ya kikristo  Nyingine zilizofuta   "The Old Order in Conflict with the New" and "Dead Men's Path"  zikielezea vita kati utamadu  na maisha ya usasa
Baada ya kuwasili  kwa  professor   Geoffrey Parrinder  katika  chuo cha Ibadan  kufundisha  Ushirikiano wa kidini , Achebe  alianza kupeleleza  juu ya chimbuko la dini ya kikristo na tamaduni za afrika.
Mwaka 1953,  achebe alifanya mt ihani wake wa mwisho  wa shahada yake ya kwanza katika chuo kiku cha  Ibadan  na   kufaulu  katika daraja la pili ambpo alirejea nyumban  kwao  Ogidi kuoangalia machagu yake.
Baada  kuhitimu elimu yake alifundisha lugha ya kiingereza katika shule ya biashaRA  Oba AMBAPO 1954 akaanza kufanya  kazi na Shirika la utangazaji La Nigeria NbC NA KUAHAMIA  LAGOS. Alifanya shughuli nyingi akiwa na shirika hili.
Katika vita vya Biafra  1967  iliyotaka kujitenn nga kwa jimbo  la Biafra Achebe  aliunga mkono vita hivyo ,alitumikia kama balozi wa watu wa taifa jipya la Biafra  ,Baadaye serikali ilishinda NA Kuchukuwa utawala wa jimbo hilo huku CHINUA kuwaombea msaada watu wa lililokuwa taifa lake.
Baada ya utawala wa Nigeria kulichukuwa jimbo hilo 1970 aliamua kuwa mwanasiasa lakini baadaye alijiuzulu kutokana kuwapo kwa mpasuko uliosababishwa na rushwa kwa uliokuwa kwa wasomi wakati huo
Katika miaka ya 1970 Chinua aliishi nchini Marekani kwa miaka mingi Ambapo 1990 alihamishia makazi  ya kudumu nchini humo baada ya kupata ajali ya gari iliyomsababishia ulemavu wa miguu
tangu mwaka 2009 mpaka mauti ilipomkuta  2amekuwa professa wa masomo ya kiafrika katika chuo kiku cha Brown  kilichopo nchini Marekani


No comments:

Post a Comment