Thursday, February 7, 2013

ASKOFU LAIZER AFARIKI DUNIA


Marehemu Laizer



Askofu wa KKKT dayosisi wa kaskazini Thomas Laizer amefariki dunia leo katika hospitali ya Celian iliyoko jijini Arusha.
Taarifa zinasema askofu huyo aliyeaga dunia alikuwa amelazwa hospitalini hapo mpaka umauti unamfika.
Ikumbukwe kuwa Askofu Laizer hakuwa tu na mchango wa kiroho kwa kanisa lake la KKKT bali ni nchi nzima kwa kuwa alikuwa akishiriki pia katika kutoa mawazo yake juu ya masuala ya siasa ya Tanzania.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE NA KAZI YA BWANA HAINA MAKOSA.

Marehemu Laizer


Hii imetokea leo jioni ikiwa ni asubuhi tu askofu mstaafu wa jimbo la Moshi ambaye alitumikia kuanzia mwaka 1985 hadi 2008 Amedeus Msarikie amefariki dunia  huko nchini kenya alikokuwa amelazwa katika hospitali moja katika jiji la Nairobi



No comments:

Post a Comment