Friday, February 1, 2013

MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UKIMWI NA UJASIRIAMALI YALIYOANZA TAREHE, 28/01/2013 MPAKA 01/02/2013

Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmedi Kipozi akihutubia washiriki wa mafunzo ya UJASIRIAMALI na UKIMWI yaliyofanyika kwa mda wa siku tano, Sky Read Hotel iliyopo mjini Bagamoyo yakitekelezwa na ASUTA(Asasi ya Uwezeshaji Tanzania) & PY(Progress the Youth Foundation) kwa udhamini wa Rapid Funding  Envelope (RFE).

Akifunga mkutano huo, Bwana Kipozi alisisitiza kuhusu ushirikiano mzuri baina ya wana Mtandao wa Vijana Bagamoyo (MVB),ASUTA &PY na wadau wote wa maendeleo ya jamii.

Aidha bwana Kipozi amewashauri vijana kutumia ujana vizuri  akisema ujana ni maji ya moto unakuja na kupita na unachangamoto nyingi, pia ujana huo huo una mazuri mengi. Hivyo ni vema vijana kutumia ujana wao kwa kuchapa kazi kwa bidii, kuongeza weledi, kuhudhuria vyuo vya mafunzo mbalimbali, kuungana kutokomeza gonjwa la ukimwi na kushadadia shughuli za maendeleo ya uchumi kama ujasiriamali.
 Mary Matitu akiimbisha wimbo wakati wa kumkaribisha Mheshimiwa mkuu wa wilaya kwenye kufunga mafunzo ya ujasiriamali. 
Washiriki wa mafunzo ya Ukimwi na Ujasiriamali waliokuwa zaidi ya 100; kama wanavyoonekana pichani  katika mafunzo yaliyowezeshwa na ASUTA & PY kwa udhamini wa RFE katika hoteli ya Sky Read  mjini Bagamoyo. 

No comments:

Post a Comment