Friday, February 1, 2013

MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAASA VIJANA NA AWASIHI KUSHADADIA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA UJASIRIAMALI

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Ndugu Ahmedi Kipozi katikati akiwa na jopo la viongozi wa Asasi ya Uwezeshaji Tanzania (ASUTA) &Progress the Youth Foundation (PY) wakipozi kwa picha mara baada ya kufunga mafunzo hayo.
(Kulia Isaac M. Issae (Mkurungezi -ASUTA), akifuatiwa na Prince Pastory (Meneja mradi ASUTA na Mkurungezi wa PY), kushoto Mchungaji James Michael Werema (Mwenyekiti ASUTA) na Adam S. Ngamba (Mhariri NIHABARISHE Gazeti na Blogu),
Washiriki wakiwa kwenye utulivu mkubwa wakisikiliza somo la mpango wa mradi,mwenye hijabu ya pinki Asha Omary Ally -Mwelimisha rika kata ya Msata wilayani Bagamoyo.
Washiriki wakipata chakula cha mchana kilichowezeshwa na TUMALE CATERING kupitia ASUTA & PY kwa udhamini wa RFE.
Pichani Saidi Zikatimu Diwani wa kata ya Talawanda, Mwenyekiti kamati ya Elimu Afya na Maji na mjumbe wa kamati ya kudhibiti UKIMWI wilayani Bagamoyo akiongea na washiriki wa mafunzo ya UKIMWI na UJASIRIAMALI.

Mheshimiwa Saidi Zikatimu aliwaomba washiriki kuzingatia mafunzo waliyopata kwa maendeleo ya jamii kwa ujumla, hivyo aliwasihi wafuate yale yote yaliyofundishwa na pia watakaporejea makwao wafundishe wengine pia ili mwisho wa siku jamii nzima imeelewa jinsi ya kudhibiti VVU na kuondokana na umaskini uliokidhiri miongoni mwa familia za kitanzania ambazo nyingi kwa aslimia kubwa hata mkate wa siku huwa hakuna uhakika, 'Alisema kupitia nguvu za Vijana na MVB yaani Mtandao wa Vijana Bagamoyo ulioundwa na ASUTA & PY inawezekana.

No comments:

Post a Comment