DC
Bagamoyo, Ndugu Ahamed Kipozi awasisitiza vijana wa Bagamoyo kuutumia vema
Ujana wao
Na
Adam Ngamba
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Ndugu Ahmed Kipozi amewasisitiza
baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo ya Ujasiriamali na UKIMWI yaliyofanyika
katika hoteli ya SKY READ kwa muda wa
wiki moja ambayo yaliwahusisha vijana wasio na kazi maalumu, wahudumu wa baa,
watumia ma ndawa ya kulevya pamoja na wa wafanya biashara wa kuhamahama.
Hayo ameyaseme wakati
alipokuwa akifunga mafunzo ya Ujasiriamali na UKIMWI yaliyo fanyika, kuanzia
tarehe 28 Januari-1, Februari 2013.
Mafunzo hayo ambayo
yalikuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali chini ya Usimamizi wa Asasi ya
Uwezeshaji Tanzania (ASUTA) na Progress the Youth Foundation zilizo chini ya
udhamini mfuko wa RAPID FUND ENVELOPE (RFE); yameonekana kupokelewa kwa furaha na Mkuu wa Wilaya pamoja na vijana walioshiriki mafunzo hayo.
Katika hutuba yake fupi
iliyotumia yapata dakika 20, Ndugu Kipozi amewasisitiza vijana kuchangamkia fursa
ya kujifunza angali bado damu inachemka na wakati wakiwa na nguvu za kufanya kazi barabara.
“
………Katika maisha kuna hatua tatu muhimu; hatua ya utoto, ujana na utu uzima.
Kila hatua inasifa na wakati wake. Lakini hatua muhimu zaidi katika maisha ni
hii ya ya pili ya ujana ambapo kijana anakuwa bado na nguvu zake zote. Na hii
ndiyo hatua ya kijana kuwa na juhudi kubwa katika kutafuta maendeleo endelevu
kwani ni hatua hii ndiyo inayotoa muelekeo wa maisha na ndiyo maana ikapewa
majina mengi kama vile ‘ujana maji ya moto’ damu inachemka na kazalika………”
Aidha Ndugu Kipozi
aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa maendeleo hayawezi kuja kama mvua,
bali ni kwa kuzingatia mambo muhimu matatu; nia au malengo, bidii na juhudi
katika kazi na maarifa ama ujuzi katika kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili
kufikia malengo.
Ndugu Ahammed Kipozi
hakusita kuidhihirisha furaha yake kwa kuipongeza ASUTA na PY na uongozi mzima
wa Asasis hiyo kwa kuonesha nia njema ya kuiunga mkono serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania katika kutekeleza sera yake ya kupunguza umasikini uliyokithiri na kuunda
ajira kwa vijana na jamii nzima ya Kitanzania.
Mkuu huyo wa wilaya ya
Bagamoyo, aliongeza pongezi zake kwa ASUTA na PY kwa kutokusahau kutoa mafunzo
dhidi ya maambukizi ya VVU/AIDS na maradhi mengine yanayo weza kuenezwa kwa njia
ya ngono isiyo salama.
Ndugu Kipozi alisema
kuwa ni muhimu sana kwa jamii hasa vijana kujifunza masuala ya afya kwani afya
ndiyo kila kitu, kwa kuwa mtu hauwezi kuelezea maendeleo ya jamii bila
kuzungumzia afya.
Mbali na hapo, Ndugu
Kipozi amewasisitiza vijana kushiriki kwa wingi pindi fursa kama hizi
zinapojitokeza kwani mtu hawezi kujifunza akiwa kajifungia ndani tu, ni lazima
ajichanganye na wenzie na kuonesha ushirikiano wa hali na mali. Na ili
kukamilsha adhima hii, mkuu huyo ameushauri uongonzi wa ASUTA na PY kutumia
mfumo jumuishi wa mawazo, ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri ama mawazo kutoka
kwa washiriki wengine na kuwashirikisha katika mipango mbalimbali ya
kimaendeleo.
Katika muendelezo wa
habari, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ndugu Kipozi aliendesha zoezi la ugawaji wa
baiskeli takribani 20 kwa baadhi ya waelimishaji rika, ambazo zilitolewa na
ASUTA na PY kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo unao simamiwa na
Asasi hiyo yenye ofisi zake hapo mjini Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment