Kutokana na vyanzo vya habari vya NIHABARISHE imehabarishwa kuwa Padri Evarist Mushi (Pichani) wa kanisa la Katoloki visiwani Zanzibar, amepigwa risasi na watu wasiojulikana na kupoza uhai wake papo hapo wakati akielekea kwenye ibada asubuhi hii katika kanisa la MTONI , ZANZIBAR. Hadi sasa sababu hasa za kupigwa risasi padri huyo bado msamiati.
Habari zaidi ni kwamba waliompiga risasi walikuwa wawili na waliibuka eneo la tukio ambalo ni karibu na kanisani hapo kwa mbwembwe za pikipiki huku wamepakizana kwenye pikipiki aina ya VESPA na Padri Evarist akiwa kwenye agri yake baada ya tukio gari lilipoteza uelekeo na kuelekea kwenye nyumba.
MUNGU REJESHA AMANI YA TANZANIA.
MUNGU BARIKI AFRIKA
MUNGU BARIKI TANZANIA MAOVU HAYA YAKOME
No comments:
Post a Comment