Washiriki wa mafunzo ndani ya THE NEW DODOMA HOTEL. |
Shirika
lisilokuwa la kiserikali Foundation for civil Society FCS leo limenza kutoa mafunzo
kwa Asasi Zisizo za Kirai (AZAKI) mjini DODOMA katika hoteli ya THE NEW DODOMA
HOTEL. Kutokana na vyanzo vya habari vya nihabarishe mafunzo hayo yatadumu kwa
siku tano kuanzia 11/02/2013-15/02/2013.
Foundatio
For Civil Society ni shirika ambalo liko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa
NGO/AZAKI zinatimiza malengo yake kwa ajili ya kusaidia jamii kukabiliana na matatizo
mbalimbali yakiwemo umaskini uliokithiri, kurekebisha sera butu, ushawishi wa
sera na utawala bora
Kwa
upande wao washiriki wa mafunzo hayo
toka sehemu mbalimbali za Tanzania wameshukuru sana kwa mafunzo hayo kuwaondoa
katika giza
“Kwa
mara ya kwanza nimefurahia kuhudhuria
mafunzo ya Foundation for Civil Society kwani ni dhahiri nilikuwa sijui umuhimu
wa hati ya malipo katika shirika letu leo hii nimejua nasikujua kuandaa
mchanganuo wa mapato na matumizi lakini leo kupitia mwalimu wa mafunzo Bwana
Tuntufye Mwaiteleke nimeyajua hayo” alisema Sister Aneth Mwani toka Emau
Development toka Njombe.
Sister Aneth Mwani akipoza kwa picha mara baada ya mafunzo hayo. |
Aidha
mshiriki mwingine bwana Godwin Maganga toka TUMAINI DISABLED COMMUNITY toka
Tabata Dar es Salaam alisema nae kafurahi pia kwa yote yaliyofundishwa juu ya
mchanganua wa fedha ndani ya asasi.
Bwana Godwin Manganga akiwa amepozo kwa picha mbele kidogo ya lango la THE NEW DODOMA HOTEL |
Kwa
upande wake mwezeshaji wa Semina hiyo Bwana Tuntufye Mwaitekele alijikita
kwenye mada za Usimamizi wa fedha, Udhibiti wa Fedha na nguzo zake kama Muundo,
Muungozo na Mfumo, aliweka bayana viashiria vya muundo madhubuti ili kuwezesha
AZAKI kuleta tija katika utekelezaji wa miradi. Pia washiriki wamewezeshwa
kujua jinsi ya kuandaa Mchanganuo wa Mapato na Matumizi ya fedha katika shirika na umuhim
wake. Kingine cha msingi Mwezeshaji aliweka bayana utenganisho wa Majukumu
ndani ya Asasi hapa ndipo maswali mengi yalimiminika toka kwa washiriki lakini
kutokana na uzoefu wa mwezesha bwana Tuntufye L. Mwaitekele aliwajibu na
kuwaelewesha vizuri alitumia ueledi wa juu na mbinu shrikishi mpaka mwisho wa
siku washiriki waliokuwa na maswali wameelewa hii ni kutokana na vyanzo vya
habari vya NIHABARISHE na uchunguzi wa kina uliofanywa na NIHABARISHE kwa njia
ya focus group discussion na mahojiano ya mtu kwa mtu (Oral Interview).
Washiriki wakiwa ndani ya ukumbi wa THE NEW DODOMA HOTEL.
No comments:
Post a Comment