Monday, December 31, 2012

IZZE MARTIN AACHIA NGOMA MPYA

Yule msanii anayekuja kwa kasi na kutishia amani ya wakongwe wa tasnia hiyo hapa nchini Kijana Izze Martin ameachia wimbo mpya uitwao HUYU akishirikiana na msanii Milyo. Ngoma hiyo according to him imekuja muda huu wa mwisho wa mwaka ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wake.
Ngoma hiyo ambayo imepokelewa vizuri  na maraia kibao wakisifia vocal za wasanii hao bila kumsahau producer akiwa ameitendea haki ngoma hiyo.



SENSA 2012 KIKWETE AONYA

 Ongezeko la idadi ya watanzania limemstua JK,  asema watu milioni 44.9 sasa ni mzigo kwa serikali, na kuwataka Watanzania kufuata uzazi wa mpango vinginevyo hali ya maisha itakuwa tete.....
Hayo ameyasema leo katika  viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam alipokuwa akitangaza matokeo hayo ya awali ambapo pia waziri mkuu Mizengo Pinda na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Seif Ali Idd imeonesha kuwa Watanzania tupo 44,929,002. ikiwa Tanzania Bara ina idadi ya watu milioni 43,625,434 huku Zanzibar wakiwa 1,303,568.
kwa upande mwingine wadau wamesema kuwa huenda idada iko zaidi ya hapo huku wakitoa sababu kuwa kuna baadhi ya Watanzania hawakuhesabiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo na wengine kukwepa kuhesabiwa kwa sababu ya imani zao. 
                  

Sunday, December 30, 2012

KEBBY'S HOTEL AN EVER SHINING RESTAURANT OF ITS TIME. HERE INTRODUCE A FAMOUS OPERA LOUNGE, THIS FRIDAY, SATURDAY & TUESDAY. KEBBY'S HOTEL HAVE COCKTAILS IN THE HOUSE SECOND FLOOR @10,000/TSHS PER GLASS .

KEBBY'S HOTEL AN EVER SHINING HOTEL OF ITS TIME. HERE INTRODUCES TO YOU A FAMOUS OPERA LOUNGE, THIS FRIDAY, SATURDAY & TUESDAY. KEBBY'S HOTEL HAVE COCKTAILS IN THE HOUSE SECOND FLOOR @10,000/TSHS PER GLASS .

YOUR WARMLY WELCOME.
PLEASE COME SHARE FUNNY AND INTERACT WITH PEOPLE FROM ALL WALKS OF THE WORLD.

HOSPITALITY AND EXCELLENCE DISTINGUISHED SERVICES IS OUR MOTTO.
















                                                                                                                  Kindly contact us 
Kebbys Hotel,
Bamaga-Mwenge, New Bagamoyo Road
P.O.Box 31156 Dar es Salaam-Tanzania
Phone:
+255 22 2774094+255 22 2774094 FREE
Fax +255 22 2773095
Email: sales@kebbyshotel.com

'2030' YA ROMA YALETA BALAA

Ule wimbo alioutoa msanii R.O.M.A siku ya ijumaa ukiwa na title 2030 umezua gumzo sehem mbalimbali ikiwemo katika mitandao ya kijamii ukihusishwa kwenda kinyume na dini ya kiislam. Wimbo huo   umeombwa kupigwa marufuku na waislam wote sababu ikiwa ni msanii Roma kusema tukio la kijana kukojolea msaafu ni sawa.....Hapa nanukuu maneno ya   Hemedy Suleiman kutoka facebook.
 


 NYIMBO MPYA YA ROMA MKATOLIKI MPYA IITWAYO "2030"
WAISLAMU TUNAIPIGA MARUFUKU DUNIA KOTE

Ameisifia na Kuuponda Uislamu pia...Wewe
kama Muisalmu kama unayo ifute na
usi Isambaze...Msahafu kukojelewa asema ni sawa
yule mtoto hajui Kanisa kwaiyo waislamu tumefanya makosa kuchoma kanisa.Ana isitoshe ametaja neno
Allah mara nyingi katika Nyimbo hiyo.

Hii siyo mara ya kwanza kwa msanii huyu kuuimba mada zake katika nyimbo zake za nyumba ameshawahi kutaja aya ya Quran katika Maafa ya Mv spice

Tuma Ujumbe
huu kwa watu wengi Kuhakikisha isisambae Hii
Nyimbo imetoka 28/12/2012.....Hakika Mnatakiwa
kuonyesha Hatua kali dhidi yake ichukuliwe Kafiri Huyu'  Mwisho wa kunukuu


ROMA

ASUTA +PY MWAROBAINI KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU BAGAMOYO

ASUTA +PY MWAROBAINI KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU BAGAMOYO :

ASUTA-Asasi ya Uwezeshaji Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linasaidia jamii katika nyanza za Afya, uchumi na kiutamaduni. ASUTA iko kihalali na imesajiliwa kwa sheria za AZAKI 2002. Kwa mradi wa kuzuia maambuikizi ya VVU Bagamoyo unaofadhiliwa na RFE, ASUTA kwa ushirikiano na Progress the Youth Foundation kwa pamoja mashirika haya yameweza kufikia makundi ya watumia madawa ya kulevya, wahudumu wa bar, wafanya biashara ya ngono na wafanyakazi wa kuhamahama. 

Awali ya yote wilaya ya Bagamoyo ina kata 22 na  ina sababu nyingi kwa maambukizi ya VVU kushamiri ikiwemo ni mji wa kitalii, mji unao kaliwa na watu wa tamaduni mbalimbali toka pande zote za dunia wakiongoza kwa kuingia na kutoka. Bagamoyo au BWAGAMOYO kwa jina asili ina bandari, kuna shughuli za uvivi, usafirishaji, uingizwaji wa tamaduni ngeni tofauti na za asili unaharibu vijana na wengi kujiingiza katika tabia hatarishi kama kufanya biashara ya Ngono, kutumia madawa ya kulevya au kuuza, kuwa na wapenzi wengi n.k. Wakati mradi uanaanza maambukizi yalikuwa 9.4% takwimu za mganag mkuu wa wilaya bagamoyo pamaoja na wizara ya Afya. ASUTA imechangia sana kupunguza maambukizi ya ukimwi ambayo yamefikia takribani 7% kutokana na ripoti iliyotolewa siku ya ukimwi dunia 01/12/2012 iliyofanyika KIJIJI CHA MDAURA JIMBO LA CHALINZE. Iliratibiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kwa ushirikiano na wadau wengine ASUTA akiwa mojawapo ya washiriki wakubwa, NIHABARISHE IMEELEZWA.
NIHABARISHE imeelezwa kuwa Bagamoyo kuna AZAKI nyingi sana hizi ni habari rasmi kutoka kwenye vyanzo vya habari vya NIHABARISHE na nyingi zilishriki siku ya ukimwi duniani AZAKI hizi ni ASUTA, PROGRESS THE YOUTH FOUNDATION, BAGEA, CVM, UWAMABA, UVIWAMABA, TWISUKA, BANGONET, AWABA n.k.

Wadau wa AZAKI hizi wameomba serikali kuongeza nguvu kifedha ili kuziwesha kutekeleza shughuli ipasavyo, NIHABARISHE limeambiwa VVU bado vipo na tatizo halijaisha kutokana sababu zilizotajwa juu. Alikaliliwa mmojwapo wa wahanga wa tatizo hili aishe Kata ya DUNDA Mitaa ya mangesani akisema hili tatizo kwa wilaya yetu namuomba Mheshimiwa Rais  wa jamhuri ya muungano aingilie kati tatizo bado kubwa, bado unyapaa upo, kuambukizana kwa makusudi na lishe kwa WAVIU hakuna aksema tunakuomba Raisi wetu utupie jicho wilaya ya Bagamoyo kutukwamua kiuchumi na kiafya. NIHABARISHE lilimkalia kitako na kunyaka yaliyo yake moyo na hakusita kumwagika kama mwandishi wetu alivyotambaa nae bila kuachia singo dot ya kilichosemwa. Hivyo NIHABARISHE linaomba wadau wote akiwemo Mheshimiwa Rais DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE na wengine sio tu RFE kusaidi wilaya hii yenye changamoto lukuki jinsi ya kufikia kauli mbiu ya ukimwi duniani: 

TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAVYO NA VVU INAWEZEKANA (TANZANIA WITHOUT NEW HIV/AIDS INFECTION, ZERO DESCRIMINATION AND DEATHS RELATED TO HIV/AIODS IS POSSIBLE.
Mmoja wa maafisa wa PY alisema REACHING TO ZERO HIV/AIDS IS POSSIBLE WITH A JOINT VENTURE YES WE CAN.

Aidha kwa robo ya kwanza ya utekelezaji iliweza kuwafikia vijana 650 walioko mazingira hatarishi, vijana hawa walipatiwa elimu elimishi jinsi ya kujikinga na VVU na ukimwi. Kutokana na vyanzo habari vya NIHABARISHE imebaini kuwa vijan hawa walikuwa hawana uelewa mzuri wa kujikinga na VVU.
''Akikaliliwa kijana mmoja mfaidika wa mradi kwa jina la Stamily Idd alisema ASUTA imenisaidia kumbe kufanya apenzi bila kondom hata kama mtu unamjua si salama sasa nimejifunza nimeelewa na nitawaelimsha na wenzangu mtaa.
ASUTA imefanya mafunzo ya waelimisha rika 50 kwa siku tano mfululizo hoteli ya SYKREAD BAGAMYO. Watu walioshiriki ni wahusika wa mradi kama wahudumu wa bar, watumia madawa ya kulevya, wafanya biashara ya ngono na wafanya kazi wa kuahamahama wakiwemo wawakilishi toka kila kata wilayani Bagamoyo. Waelimisha rika hawa wataelimisha watu wengine zaidi nainakadiliwa kuwa kila mtu hueimisha zaidi ya watu 100 kwa robo ya mradi aidha ripoti ndani ya shirika baada ya nihabarishe kuchimba kwa kina na kiutafiti zaidi ilijulikana kuwa mojawapo ya waelimisha rika wameweza kufikia watu zaidi ya 1000 kwa mwezi mfano mwelimisha rika toka kata ya Msoga ambapo mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ndiyo kata ya nyumbani ameweza kufikia idadi ya watu zaidi ya 1000 kuelimisha kuhusu maambukizi ya VVU akishirikiana na mwezake Juliana.

Kwa kata ya chalinze ASUTA ina wapinaji wazuri katika kutokomeza maambukizi mapya ya VVU ambao wanatoa ripot kila robo ya utekelezaji na kila mwezi Bwana Charles Manganga na Abdallah Tiff Shabani wamesaidia sana kusambaza uelewa jinsi ya kujikinga na VVU kwa makundi ya watu walioko mazingira hatarishi.
ASUTA imenunua baiskeli na kugawa kwa waelimisha rika yaani  PHE'S, kwa mradi wa kuzuia maambukizi mapya ya VVU ROUND 9 Chini ya udhamini wa RFE na inaendelea kuwagawi kurahisha utekelezaji wa mradi. Fuatilia ripoti kamili toleo lijalo kutakuwa na vielezo na takwimu zaidi.

PICHA CHINI NI WAKATI WA MATAMASHA YA KUZUIA VVU BAGAMOYO HAPA NI CHALINZE TIMU YA MPIRA, WA KWANZA KULIA MENEJA MRADI NA MWENYE SHATI JEUSI NI DIWANI KATA YA CHALINZE

 KUZUI VVU, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAYO NA VVU NI LAZIMA MBINU NA MIKAKATI MINGI IHUSISHWE. KAULIMBIU YA MCHEZO MPIRA KWA NGONO SALAMA NA MICHEZO YOTE KWA NGONO SALAMA ILI TUFIKIE MALENGO YA MDG.
 CHINI TIMU YA MPIRA JEZI BLUE KWA JINA LA MAVAMPIRE FC VS CHALINZE VETERANI FC KUZUIA VVU BAGAMOYO NA TANZANIA KWA UJUMLA.
MABANGO YENYE UJUMBE ELIMISHI, ASUTA+PY WAMESAMBAZA MABANGO HAYA MAENEO MENGI YA BAGAMOYO KWENYE AKUTANO YA WATU KWA AJIRI YA KUZUI VVU
 VIJANA MAHIRI TOKA TOT WAKICHEZA NGOMAMUZIKI WENYE UJUMBE WA KUKINGA VVU BAGAMOYO WAKIONGOZWA NA NURDINI PAMOJA NA LETICIA KUELIMISHA NA BAADAE KUSHIRIKI UGAWAJI KONDOM NA TSHIRT ZENYE UJUMBE KUZUIA VVU 2012/08-10.
VIJANA KATIKA MAZUNGUMZO YA MASWALI NA MAJIBU KWA UHURU KWA KILA MTU KUCHANGIA FOCUS GROUP DISCUSSION & OPEN DIALOGUE.

 MAAFISA WA ASUTA WAKIWA NA WEO KATA MANDERA KWENYE UGAWAJI WA KONDOM, VIFAA ELIMISHI IKIWEMO SANAMU YA UUME, VIPEPERUSHI, KONDOM NA HUKU WAKITEKELEZA ZOEZI LA TATHIMNI M&E.
  MAAFISA WA ASUTA WA KWANZA KULIA MWENYEKITI ASUTA AKIJITOLEA KUTEKELEZA KAZI ZA MRADI AKIMKABIDHI BI MAENDELEO KATA YA LUGOBA KWENYE UGAWAJI WA KONDOM, VIFAA ELIMISHI IKIWEMO SANAMU YA UUME, VIPEPERUSHI, KONDOM NA HUKU WAKITEKELEZA ZOEZI LA TATHIMNI M&E YA MRADI 2012/06-07.
 AFISA WA ASUTA BWANA RAMADHANI SALUM  HIZA WAKATI WA UTAFITI MDOGO MWANZONI MWA MRADI SHUGHULI YA 1.2 . UTAFITI HUU ULIKUWA NA MALENGO YA KUJUA HALI HALISI YA VVU NA KUWATAMBUA WALENGWA MAPRS/WATU WALIOKO MAZINGIRA HATARISHI KWA MAJINA NA KUWAORODHESHA ILIFANYIKA KATI YA MWEZI WA 04/2012-05/2012
 BI MAENDELEO LUGOBA AKIPOKEA MABOX YA KONDOM KWA AJIRI YA WATU WA KATA YAKE KUTOKA KWA MOJAWAPO YA MAAFISA WA ASUTA MENEJA MRADI PRINCE PASTORY.

 BI MAENDELEO LUGOBA AKIPOKEA VITABU MIONGOZO YA WAELIMISHA RIKA KWA AJIRI YA WATU WA KATA YAKE NA WAELIMISHA RIKA WAKE KWA KATA YAKE ASUTA IMEFUNDISHA WAELIMISHA RIKA WAWILI.

 BI MAENDELEO LUGOBA AKIENDELEA KUPOKEA VIFAA ELIMISHI TOKA ASUTA +PY
 WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUZIA UKIMWI MSOGA WAKIPOKEA DHANA MAALUM KWA KUZUIA VVU TOKA ASUTA

 WA KWANZA KULIA MKURUNGEZI WA ASUTA AKIWA NA MWELIMISHA RIKA WA  KATA MAGOMENI MS NEZIA MANYAMA WAKIWA FIELD MAENEO YA UTENDAJI KAZI WAKIWATEMBELEA WALENGWA. AIDHA WALIWEZA KUWAFIKIA WALENGWA WENGI NA KUCHANGUA KIONGOZI WAO AMBAYE NI FARIDA ALLY RUBA AMBAYE MRADI UMEMSAIDIA AMEACHA TABIA HATARISHI, AMEELIMIKA NA ANAELIMISHA WENGINE NA AMEWEZA KUFIKIA WATU ZAIDI YA 190 WALIOKO MAZINGIRA HATARISHI NIHABARISHE ILIELEZWA. PIA FARIDA ALLY RUBA  ALIWEZA KUPATA MAFUNZO YA SIKUN TANO 2/5/2012-6/05/2012 SYKREAD HOTEL NA ALIKIRI KUWA YAMEMSAIDIA NA AMEBADIRIKA SANA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI
ASUTA
SLP 70
BAGAMOYO
Barua pepe: asutatz@gmail.com
Mob:+255754 464 393/754941134



                                                    PROGRESS THE YOUTH FOUNDATION
      Barua pepe: progresstheyouth@gmail.com
      Mob: +255712 328 862

WISDOM

IS IT A SAYING OF THE WISEST?

Saturday, December 29, 2012

TUDUMISHE MAADILI NA TAMADUNI ZETU TAFADHALI,,ONA WENZETU SASA NI KUDUMISHA MAADILI KWA KWENDA MBELE SIO NYUMA



TUDUMISHE NA TUENDELEZE MAADILI YETU. AWE MTZ HUDHURIA NA JUMUIKA NA WENZAKO TUDUMISHE TAMADUNI ZETU KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.

MABINTI WAENDESHA BODA BODA NA WAZICHANGA BALAA USIPIMEE ZAMA.SASA....: AMKA.....!!!..? HAKI SAWA NA FURSA SAWA KWA WOTE, WANTANZANIA MKO WAPI? BADO MNALILIA VITI MAALUM? NI KWELI SOTE TWAWEZA?

YANAYOJIRI KENYA. 

JE TZ BADO MNALILIA VITI MAALUM TU? 
JE VITI MAALUM LAZIMA? JE SOTE TWAWEZA?
 JE BADO TUNA ULAZIMA WA KUBAGUA AU KUCHAGUA KAZI?
KAMA ALIVYOJISEMEA JOYCE WA KINONDONI NAFANYA KILA KITU LAKINI LABDA KUCHIMBA KABURI TU .........ALIONGEZEA LAKINI HATA HIVYO IKIBIDI NAPASUKA NALO TU SO ISSU MZAZI..............MWANAMKE PEKEE HABAGUI JOB, ILI MRADI MKONO UENDE KINYWANI KIUHALALI.................ALIKARIRI AKIBWATA KWA SPIDI KALI BAADA YA KUWA AKERWA NA WANAWAKE PAMOJA NA VIJANA WA KUME WANAOJIMODOSHA NA KUCHAGUA KAZI ALISEMA NA KUMALIZA HIYO SO ISU MZAZI.

NIHABARISHE TAREHE 29/12/2012 KINONDONI MANYANYA, DSM.

NDANI YA ARIDHI YA KENYA WANAWAKE WASUKUMA GURUDUM KWA KASI??????????

NIHABARISHE KUTOKANA NA VYANZO VYAKE VYA HABARI IMEFUMA LIVE HABARI HII BILA CHENGA ENDELEA NA UTOE MAONI?

Picha ya teksi ya pikipiki ya Faith Kabura Makena kwenye barabara za Garissa nchini Kenya inatoa taswira ya nadra sana.
 Grace Ruwa Asar, mwanamke wa kwanza kuwa dereva wa bodaboda Kenya, akimbeba abiria kwenye eneo la Tana River Delta. [Bosire Boniface/Sabahi]

Faith Kabura Makena alivunja kikwazo cha kijinsia kwa madereva wa kike wa bodaboda mjini Garissa. [Bosire Boniface/Sabahi].
Makena, mwenye umri wa miaka 30, alisema anajua kwamba kuchagua kwake biashara hii kumesababisha utata na mara kadhaa huwashangaza wakaazi wa huko anapowapita.
Teksi za pikipiki, zinazojulikana kama bodaboda nchini Kenya, ni njia maarufu ya usafiri kwa wasafiri wanaotaka kukwepa foleni kubwa za magari mijini. Wakati inatoa fursa ya kupata maisha mazuri kwa waendeshaji wake, hii ni biashara ambayo imekuwa ikitawaliwa na wanaume tu.
Hata hivyo, Makena alisema aliamua kuipa changamoto imani iliyopo na kuwa dereva wa bodaboda kwa sababu ni chanzo kizuri cha mapato ya kumuhudumia mtoto wake wa kiume wa miaka 6 na wazazi wake, ambao ana jukumu la kuwatunza kifedha.
"Mwanzoni nilikuwa ninakerwa na namna watu walivyonichukulia lakini kutokana na uungaji mkono wa familia yangu na marafiki, nilisonga mbele," aliiambia Sabahi. "Wiki za mwanzo zilikuwa ngumu kwa sababu sikuweza kupata wateja. Mteja mmoja hata aliwahi kuniambia kwamba nilikuwa ninatania na asingeliweza kuamini usalama wake barabarani kwenye mikono ya dereva mwanamke."
Makena alisema kwamba binamu yake alimfundisha kuendesha pikipiki kwa nia ya kujifurahisha tu. "Kutokana na uchache wa ajira, ilinipitikia kwamba kile nilichojifunza kwa kujifurahisha kinaweza kuwa fursa za kuzalisha kipato," alisema.
Makena, ambaye mwanzoni alikuwa akimiliki duka, amekuwa dereva tangu mwezi Januari, akiwa kwa wastani anapata shilingi 20,000 (dola 233) kwa mwezi. Kwa sasa anafanya kazi na dereva mwingine lakini anatarajia kuweka akiba hadi shilingi 80,000 (dola 931) kufikia mwezi Februari ili aweze kununua pikipiki yake mwenyewe na kuwa dereva anayejitegemea.
Lengo lake kuu, hata hivyo, ni kuwa mwalimu wa sekondari ya juu. Makena alisema amekuwa akiweka fedha kila mwezi kulipia shule, ambako ataanza mwezi Juni ujao.
Mwenyekiti wa Chama cha Boda Boda wa Garissa Joseph Musili aliiambia Chanzo cha NIHABARISHE cha habari kwamba waendeshaji wengine wengi walikuwa na mtazamo mbaya wakati Makena alipoanza kuingia kwenye biashara hiyo.

"[Kusitasita huko] kulikuja kwa sababu yeye ni mwanamke," aliiambia Sabahi. Lakini jumuiya hiyo iliwaelimisha wanachama hao kwamba ikiwa wanaume wanaweza kuwachukua wanawake kwenye bodaboda, basi wanawake pia wanaweza kuendesha. "Hilo [hatimaye] liliingia kwenye akili zao na kila mtu anafahamu na anamkubali mmoja wetu."

Ben Njogu, mwenye umri wa miaka 31, mkaazi wa Garissa, aliiambia chanzo cha habri cha NIHABARISHE kwamba mwanzoni aliamua kubebwa na bodaboda ya Makena kwa udadisi tu. "Udadisi ukawa tabia, na sasa mara kwa mara humtafuta kunipeleka safari zangu, labda awe hayupo [kazini]," alisema.
Ifrah Ali Masha, mkaazi wa Garissa mwenye umri wa miaka 24, aliiambia Chanzo cha NIHABARISHE cha habari  kwamba alishituka alipomuona mwanamke akiendesha bodaboda.

"Kwa mwanamke kuanzisha hatua hama hiyo ya kibiashara ni dalili kwamba kila wanaume wanachoweza kukifanya, wanawake wanaweza pia kama wakipewa nafasi," alisema. Pamoja na hayo, Makena anatoa huduma kwa wanawake ambao wanaogopa madereva wa kiume aidha kwa sababu za kiusalama au kimila, alisema Masha.
Makena anaripotiwa kuwa mwanamke wa pili kuingia kwenye biashara ya boda boda nchini Kenya, baada ya Grace Ruwa Asar wa Tana River Delta.
Asar, aliyeanza kuendesha boda boda mwaka 2010, alisema kwamba alilazimika kupambana na hofu zake dhidi ya mitazamo ya watu ili kujiwezesha kiuchumi.
"Ni biashara nzuri sana ambayo naweza kupata zaidi ya shilingi 50,000 (dola 582) kwa mwezi baada ya kutoa gharama kama za mafuta na matengenezo," aliiambia chanzo NIHABARISHE cha habari.
Jamii ya Kenya yenye kuelemea ubabani ina fursa chache za kibiashara kwa wanawake, alisema Asar. "Wanawake wanapaswa kuchukua jitihada zao wenyewe na kujiamini," alisema.
Kutokana na kipato chake cha boda boda, Asar anaweza kujihudumia mwenyewe na kaka zake wawili ambao bado wanasoma.
Ufunguo wa kuingia kwenye biashara hii, anasema, ni kuwa na maadili sana, hasa kuwapuuzia wateja wa kiume ambao wanamfananisha mwanamke aliyeingia kwenye biashara iliyotawaliwa na wanaume na mwanamke asiye na maadili.
"Wanaume wengine hudhani kwamba huna heshima unapowabeba," alisema. "Nililazimika kumpiga kibao mmoja wa wateja wangu wa kiume ambaye alinitomasatomasa." Hata hivyo, alisema kuwachukulia wateja wake kidiplomasia kulimsaidia kuwa na mahusiano mema na wateja.

JE NIHABARISHE LINAULIZA MAONI YAKO UNAWAAMBIA NINI WA TZ?


THE SCRET OF SUCCESS...........SEE, GRAB IT NOW.


IMELETWA KWENU NA

 ETERNITY GOSPEL FORUM.









IMEDHANIWA NA





NANI KAMUIGA MWENZAKE? WHO IS THE FOUNDER OF THE STYLE?


KUMBE KUNA KUIGANA KUANZIA WALKING STYLE MPAKA STYLE ZA MAMBO MENGINE AMA KWELI HII KUMBE NI YA WANYAMA PORI AU WANYAMA PORI WAMECHUKUA KWA BINADAMU?



BE YOURSELF YATAKUSHINDA MWISHO WA SIKU........................................................????????????????

A BIT FUNNY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



JUMAPILI NJEMA. IFANYE KUWA NJEMA KWELI SHARE PLZ.

ASETI YAKO KUBWA NI NINI KWA HAPA DUNIANI? NA JE KWA MBINGU? NA UWE MFANO?

Thursday, December 27, 2012

JIAJIRI NA AJIRI NA WENGINE ZAIDI. {JUA JINSI YA KUANZISHA SACCOS/MICRO FINANCE/VIKOBA}

Chama cha ushirika wa akiba na mikopo SACCOS ni asasi ysa kifedha inayoundwa na watu waliojiunga paomaja kwa hiari yao ambao wamekubaliana kuweka fedha zao kwa pamoja na kukopeshana kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi, kitamaduni na kijamii kwa ujumal ili kuleta ustawi bora wa jamii zao.

MISINGI YA USHIRIKA: (CO-OPERATIVE PRINCIPLES)
Ndugu mpendwa msomaji leo tutaanza kutaja aina za misingi ya ushirika ambayo ikufuatwa huimarisha kwa 100% na tofauti na hapo ushirka hukumbwa na dhoruba pamoja na majanga ya ajabu na hatimaye anguko lake, misingi hii ni kama ifuatavyo. fuatilia toleo lijalo mda si mrefu kwa ufanuzi uliotukuka na kwa kuwachanganua wenzetu nguli katika hii fani na wenye tafiti zilizo kaa sawa kama ALEXANDREAW CHAYONOUF kutoka urusi aliyesoma na kufnya na ushirka kwa mda mrefu na hatimaye akaandika kitabu chake kinachoenda kwa jina la THE PRINCIPLES OF CO-OPERATIVES.
1.UNACHAMA ULIO WAZI NA HIARI.
..............
2.UTAWALA WA DEMOKRASIA
3.USHRIKI WA MWANACHAMA KATIKA UCHUMI
4.UHURU WA KUJITEGEMEA
5.ELIMU MAFUNZO NA HABARI
6.USHRIKIANO BAINA YA VYAMA VYA USHIRIKA
7.HUDUMA KWA JAMII.

ITAENDELEA TOLEO LIJALO......
UHAKIKA NA FAIDA ZAKE :
BAADA YA KUFATILI VIZURI KWA KINA UTAWEZA KUJIAJIRI MWENEYEWE NA KUAJIRI WENGINE ZAIDI TUSAIDIE KUTEKELEZA ILANI NA MALENGO YA SERIKALI YETU.

IMELETWA KWENU NA Fabulous Consulting Ltd.







ROMA KUACHIA NGOMA '2030'

Yule msanii machachali kila mahali ikiwa ni jukwaani au kusikiliza ngoma zake R.O.M.A anakuja na ngoma mpya ambayo itatoka kesho ijumaa tarehe 28 mwezi wa kumi na mbili. Jina la wimbo ikiwa ni kama kawaida yake R.O.M.A lina utata kwa mtu yeyote atakayelisikia kwa mara ya kwanza kwa sababu ni wimbo uitwao 2030............msanii huyo amesema ataelezea zaidi wimbo huo ukitoka lakini ni mwendelezo wa falsafa yake ya MATHEMATICS akisema kajaaliwa kupata mtoto mwaka huu na atakuwa mtu mzima 2030. so raia wanasubiria sana hapo kesho kuzama you tube kama mwenyewe atauweka you tube ili wausikie mashairi yake, lakini pia na uongozi wa blog hii utakupa data zaidi hapo kesho.

Wednesday, December 26, 2012

TAMRA YATOA ONYO

 
TAMRA YAONYA WANAUME WAZINGATIE SHERIA ZA NCHI VINGINEVYO WANAUME WAKOROFI HAITAWASAIDIA
Na - SELEMANI PHARLES MABALA - DAR ES SALAAM
Chama cha kutetea haki za Wanaume Tanzania TAMRA kimewataka Wanaume kote nchini kuzingatia sheria za nchi na kuacha mara moja kuonyesha ubabe kwa kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wanawake wakati wakiwa wametenda makosa mbalimbali majumbani mwao vinginevyo hakitakuwa tayari kumlinda mwanaume yeyote ambaye atakuwa amekwenda kinyume na matakwa ya chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa na viongozi wa chama hicho nchini akiwemo mwenyekiti wa chama hicho nchini Bwana Belensi Alkadi na  Katibu Mkuu wa chama hicho nchini Bwana Antony Sollo walipokuwa wakizungumzia hoja mbalimbali pamoja na changamoto zinazowakabili wanaume mbalimbali nchini.
Bwana Sollo amesema wanaume hukumbana na matatizo makubwa katika familia zao lakini hakuna namna nyingine itakayosaidia kuidumisha amani ndani ya familia hizi isipokuwa wanahitaji kuwa wavumilivu,na zaidi ya yote watumie busara zaidi,hekima zaidi katika kuyamaliza masuala mbalimbali na changamoto za wanandoa kwa vile hakuna kitu kinachomkuta mwanandoa kwa bahati mbaya bali hatua ya kwanza ni kukumbuka kuwa wanandoa hawa waliapa viapo vya utii kwa mungu wao siku ya ndoa yao viapo hivi vinakwenda sambamba na uvumilivu katika mambo mbalimbali ikiwemo umaskini,utajiri, magonjwa na mambo mengine ya aina hiyo ambapo bwana Sollo ameshangazwa na tabia ya mmoja wa wanandoa kufikia kumlalamikia mwenzake kuwa ameshindwa kuvumilia shida za mwenzake na kwa sasa hana uwezo tena wa kuendelea kuishi na mtu ambaye hawezi kumtunza na kuamua kuivunja ndoa bila ya kuwashirikisha hata viongozi wa dini pamoja nan wazazi ambao ni mojawapo wa waliobariki na kutoa kibali cha wawili hawa kuishi kama mme na mke.
Naye Mwnyekiti wa chama hicho nchini akizungumzia hali ya mifarakano ya kifamilia amesema kuwa moja ya vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa matatizo katika ndoa na kupelekea kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani ni pamoja na mmomonyoko wa maadili ya Mtanzania kwa vile baadhi ya familia zimekuwa na majukumu ya kujitafutia maisha huku zikiwaachia watumishi kulea watoto bila kushiriki kwa wazazi kufundisha malezi bora kwa watoto,maendeleo ya Sayansi na teknolojia kwa vile kwa sasa watoto hujua haraka mambo makubwa ambayo umri ulikuwa haujafikia kuyajua na kuyatenda  jambo linalosababisha kupungua kwa kasi kubwa kwa heshima katika jamii.
 Akizungumzia malezi na makuzi ya kipindi kilichopita Bwana Sollo amesema kuwa zamani watu walikuwa hawawezi kuzungumza juu ya mambo ya mahusiano ya kindoa tofauti na ilivyo sasa ambapo tafiti zinaonyesha kuwa watoto wengi kuanzia shule za msingi na sekondari huanza mahusiano ya kimapenzi mapema na matokeo yake kushusha kiwango cha Elimu kwa kuwa mapenzi na shule ni sawa na kulima huku ukishindwa kupalilia na hatimaye kwa sababu ya kujitetea tu mtu anasema kuwa kuna uchawi umefanyika na kupelekea kushindwa kwake kuvuna mazao.
Hata hivyo akizungumzia changamoto walizo nazo wanandoa hasa wa kiume ni juu ya umaskini na hata kipato, kwa vile kwa sasa baadhi ya wanaume wamekuwa wakipambana na matatizo makubwa baada ya kushindwa kumudu maisha kufuatana na changamoto zinazowakabili ikiwamo kukosa kipato, ugonjwa sugu kama mabusha matende,Ukimwi HIV/AIDS na mambo mengine kama hayo.
TAMRA Imejipanga kukabiliana na changamoto hizi kwa kutoa elimu kwa mwanaume wa Tanzania pamoja na mototo kiume ili kuondoa dhana ya mfumo dume katika kuweka haki sawa kwa wote,amewaomba wanaume kuwa na subira na kuacha kujichukuliasheria mkononi kwa vile endapo watatenda mambo yaliyo kinyume na malengo ya chama hiki hawatakuwa tayari kuwatetea wanaume ambao watakiuka haki za binadamu kwa vile watakuwa wamevunja kanuni taratibu sheria pamoja na katiba inayoongoza nchi.
Nikweli yapo mambo yanayofanyika kwa uonevu lakini TAMRA iko macho sana kulinda na kutetea haki sawa kwa wote kwa vile siku ya Alhamisi wiki hii Katibu mkuu baada ya kuhojiwa na kituo cha ITV aliacha namba za mawasiliano na hatimaye alipigiwa simu kutoka Mkoa wa Geita ambako alipewa taarifa ya mtu mmoja ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa sungusungu kwa masaa kadhaa akisubiri kusurubishwa na alipopata wasaa wa kwenda kujisaidia tu aliomba msaada wa simu na kupata nafasi ya kuongea  na katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo ambapo Katibu huyo baada ya kupata maelezo aligundua ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo  aliwaagiza sungusungu hao kumuachia mkara moja Bwana Malimi mkaazi wa Kabuhima Runzewe Mkoani Geita na baada ya hapo walitoa taarifa kuwa tayari Bwana Malimi yuko nje na hivyo suala lake litafikishwa panapohusika.
Akielezea tukio hilo Katibu Mkuu wa TAMRA anasema, ilikuwa saa kumi jioni nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa yeye ni Bwana Malimi kutoka kijiji cha Kabuhima  Runzewe Mkoani Geita ambapo yeye alikuwa ameenda kwenye mihangaiko yake tangu asubuhi ,cha kushangaza aliporudi tu alimkuta mke wake amelewa chakali na watoto wake hawajala chakula tangu asubuhi na alipouliza kulikoni akajibiwa kuwa mimi9 siyo House Girl wa familia hiyo na kama anaona vipi aende kutafuta House Girl atakayekuwa mtu wa kuhudumia familia hiyo jambo lililomfanya agadhabike na kumpiga kofi mke wake na baada ya muda mfupi mama huyo alipiga simu mara walitokea watu walikuja na kumkamata Bwana Malimi na kumpeleka ofisi ya sungusungu na kumuweka chini ya ulinzi  ambapo mwenyekiti wa sungusungu aliomba watoe fedha kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yao ambapo mama huyo alitoa shilingi elfu themanini papo kwa papo huku akimuacha hoi mmewe kwa vile alikuwa hajui fedha hizo mkewe alizitoa wapi na hivyo alishinikiza akae rumande hadi siku inayofuata ambapo baada ya kituo cha ITV kurusha moja kwa moja mahojiano na Katibu Mkuu wa chama hicho ndiko kulipelekea ukombozi wa Bwana Malimi na Amewataka wanaume kote nchini kukiunga mkono na kukiamini chama hiki kuwa ni ukombozi wa mwanaume na ni mlinzi wa Haki za Binadamu dhidi ya ukiukwaji wa sheria na kanuni za nchi.
Baadhi ya wananchi wamekipongeza kituo cha ITV kwa kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamiin ya Watanzania nchini kwa kuita watu mbalimbali kituoni hapo ili kuzungumzia masuala mbalimbali ambayo yana faida kwao na wamevitaka vituo vingine viige mfano huu ili Taifa letu liendelee kuidumisha Amani yetu kuiweka nchi katika utulivu na usalama.

Mwenyekiti wa TAMRA Bwana Belensi Alkadi akisikiliza mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu katika Hotel ya White Sands Resort jijini Dar Es Salaam


 

Katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo wa kwanza kushoto akiwa na baadhi ya wanasheria wa Chama cha kutetea Haki za Wanaume katika Hotel ya White Sands Resort Jijini Dar Es Salaam


 
Mwanasheria wa TAMRA Bwana Ben Shebakaki akiwa katika mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Hotel ya White Sands Resort jijini Dar Es Salaam