ISAPOTI, IPENDE......
KAULI YA MWENYEKITI MTENDAJI.
Tanzani
ni kati ya nchi mojawapo zilizokumbwa na mtikisiko au anguko kubwa la uchumi
zikiwemo bei za vitu kupanda bila kukoma na huku huduma za kijamii zikizorota.
Kadhalika serikali pamoja na sekta binafisi kuwa zimefinywa na upepo huu mgumu
kushindwa kupanua ajira zinazoweza kukidhi mahitaji ya vijana wengi
wanaozalishwa na vyuo kila kukicha.
Hii
imesababisha hali ya vijana kuwa mbaya kila kukicha kutokana na kuhitimi elimu
ya juu na kukosa ajira. Vijana wamekuwa katika msongo wa mawazo wengi wao
kujiingiza kwenye shughuli hatarishi katika maisha yao zikiwemo ulevi
ulokithiri, utoaji mimba, umalaya, uuzaji madawa ya kulevya, wizi na cha
kushangaza zaidi, jinsia isiyotegemewa kufanya biashara ya Ngono nayo imeanza
kwa kasi hawa si wengine ni vijana wetu wa kiume kujiuza kwa majimama yenye
fedha yawalee au kuwaweka sawa hapa mjini Dar Es Salaaam na miji mingine. Hii
imesabababishwa na kukosa matumaini ya maisha kutokana na ukosefu wa kazi baada
ya kuhitimu masomo wakati Sera ya habari inawalinda, sera ya Vijana inawalinda
na Sera ya Uwekezaji inawalinda:
NIHABARISHE
inaleta sura mpya na suruhu ya haya matatizo lisapoti lipende na 10%
inachangiwa kwa watoto wanaaoishi mazingira hatarishi ambao pia ni matokeo ya
haya matatizo.
NIHABARISHE
litatoa kipaumbele kuajiri na kushirikisha moja kwa moja vijana wenye ueled
kupata ajira.
Aidha
litaonya na kufundisha maadili kufuatwa hata kama ugum wa miasha umekithiri
kwani suluhu huwa ipo tu pindi nguvu zinapounganishwa kwa pamoja yaani,
serikali, watu binafsi, mashirika mbalimbali kwa pamoja tunaweza kufanya
changamoto kuwa fursa zinazong’aa na si kumcha mheshimiwa Raisi au kikundi
Fulani tu kutetea jambo hii. Tukisoma sera zetu vizuri tutweza kufanisha haya
yote, kwa pamoja tunaweza
Prince Pastory
No comments:
Post a Comment