TAMRA YAONYA WANAUME WAZINGATIE SHERIA ZA NCHI VINGINEVYO WANAUME WAKOROFI HAITAWASAIDIA
Na - SELEMANI PHARLES MABALA - DAR ES SALAAM
Chama
cha kutetea haki za Wanaume Tanzania TAMRA kimewataka Wanaume kote
nchini kuzingatia sheria za nchi na kuacha mara moja kuonyesha ubabe kwa
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wanawake wakati wakiwa
wametenda makosa mbalimbali majumbani mwao vinginevyo hakitakuwa tayari
kumlinda mwanaume yeyote ambaye atakuwa amekwenda kinyume na matakwa ya
chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa na viongozi wa chama hicho nchini akiwemo mwenyekiti wa chama hicho nchini Bwana Belensi Alkadi na Katibu
Mkuu wa chama hicho nchini Bwana Antony Sollo walipokuwa wakizungumzia
hoja mbalimbali pamoja na changamoto zinazowakabili wanaume mbalimbali
nchini.
Bwana
Sollo amesema wanaume hukumbana na matatizo makubwa katika familia zao
lakini hakuna namna nyingine itakayosaidia kuidumisha amani ndani ya
familia hizi isipokuwa wanahitaji kuwa wavumilivu,na zaidi ya yote
watumie busara zaidi,hekima zaidi katika kuyamaliza masuala mbalimbali
na changamoto za wanandoa kwa vile hakuna kitu kinachomkuta mwanandoa
kwa bahati mbaya bali hatua ya kwanza ni kukumbuka kuwa wanandoa hawa
waliapa viapo vya utii kwa mungu wao siku ya ndoa yao viapo hivi
vinakwenda sambamba na uvumilivu katika mambo mbalimbali ikiwemo
umaskini,utajiri, magonjwa na mambo mengine ya aina hiyo ambapo bwana
Sollo ameshangazwa na tabia ya mmoja wa wanandoa kufikia kumlalamikia
mwenzake kuwa ameshindwa kuvumilia shida za mwenzake na kwa sasa hana
uwezo tena wa kuendelea kuishi na mtu ambaye hawezi kumtunza na kuamua
kuivunja ndoa bila ya kuwashirikisha hata viongozi wa dini pamoja nan
wazazi ambao ni mojawapo wa waliobariki na kutoa kibali cha wawili hawa
kuishi kama mme na mke.
Naye
Mwnyekiti wa chama hicho nchini akizungumzia hali ya mifarakano ya
kifamilia amesema kuwa moja ya vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa
kutokea kwa matatizo katika ndoa na kupelekea kuongezeka kwa idadi ya
watoto wa mitaani ni pamoja na mmomonyoko wa maadili ya Mtanzania kwa
vile baadhi ya familia zimekuwa na majukumu ya kujitafutia maisha huku
zikiwaachia watumishi kulea watoto bila kushiriki kwa wazazi kufundisha
malezi bora kwa watoto,maendeleo ya Sayansi na teknolojia kwa vile kwa
sasa watoto hujua haraka mambo makubwa ambayo umri ulikuwa haujafikia
kuyajua na kuyatenda jambo linalosababisha kupungua kwa kasi kubwa kwa heshima katika jamii.
Akizungumzia
malezi na makuzi ya kipindi kilichopita Bwana Sollo amesema kuwa zamani
watu walikuwa hawawezi kuzungumza juu ya mambo ya mahusiano ya kindoa
tofauti na ilivyo sasa ambapo tafiti zinaonyesha kuwa watoto wengi
kuanzia shule za msingi na sekondari huanza mahusiano ya kimapenzi
mapema na matokeo yake kushusha kiwango cha Elimu kwa kuwa mapenzi na
shule ni sawa na kulima huku ukishindwa kupalilia na hatimaye kwa sababu
ya kujitetea tu mtu anasema kuwa kuna uchawi umefanyika na kupelekea
kushindwa kwake kuvuna mazao.
Hata
hivyo akizungumzia changamoto walizo nazo wanandoa hasa wa kiume ni juu
ya umaskini na hata kipato, kwa vile kwa sasa baadhi ya wanaume
wamekuwa wakipambana na matatizo makubwa baada ya kushindwa kumudu
maisha kufuatana na changamoto zinazowakabili ikiwamo kukosa kipato,
ugonjwa sugu kama mabusha matende,Ukimwi HIV/AIDS na mambo mengine kama
hayo.
TAMRA
Imejipanga kukabiliana na changamoto hizi kwa kutoa elimu kwa mwanaume
wa Tanzania pamoja na mototo kiume ili kuondoa dhana ya mfumo dume
katika kuweka haki sawa kwa wote,amewaomba wanaume kuwa na subira na
kuacha kujichukuliasheria mkononi kwa vile endapo watatenda mambo yaliyo
kinyume na malengo ya chama hiki hawatakuwa tayari kuwatetea wanaume
ambao watakiuka haki za binadamu kwa vile watakuwa wamevunja kanuni
taratibu sheria pamoja na katiba inayoongoza nchi.
Nikweli
yapo mambo yanayofanyika kwa uonevu lakini TAMRA iko macho sana kulinda
na kutetea haki sawa kwa wote kwa vile siku ya Alhamisi wiki hii Katibu
mkuu baada ya kuhojiwa na kituo cha ITV aliacha namba za mawasiliano na
hatimaye alipigiwa simu kutoka Mkoa wa Geita ambako alipewa taarifa ya
mtu mmoja ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa sungusungu kwa masaa kadhaa
akisubiri kusurubishwa na alipopata wasaa wa kwenda kujisaidia tu
aliomba msaada wa simu na kupata nafasi ya kuongea na
katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo ambapo Katibu huyo baada ya
kupata maelezo aligundua ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo aliwaagiza
sungusungu hao kumuachia mkara moja Bwana Malimi mkaazi wa Kabuhima
Runzewe Mkoani Geita na baada ya hapo walitoa taarifa kuwa tayari Bwana
Malimi yuko nje na hivyo suala lake litafikishwa panapohusika.
Akielezea
tukio hilo Katibu Mkuu wa TAMRA anasema, ilikuwa saa kumi jioni
nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa yeye ni Bwana Malimi
kutoka kijiji cha Kabuhima Runzewe
Mkoani Geita ambapo yeye alikuwa ameenda kwenye mihangaiko yake tangu
asubuhi ,cha kushangaza aliporudi tu alimkuta mke wake amelewa chakali
na watoto wake hawajala chakula tangu asubuhi na alipouliza kulikoni
akajibiwa kuwa mimi9 siyo House Girl wa familia hiyo na kama anaona vipi
aende kutafuta House Girl atakayekuwa mtu wa kuhudumia familia hiyo
jambo lililomfanya agadhabike na kumpiga kofi mke wake na baada ya muda
mfupi mama huyo alipiga simu mara walitokea watu walikuja na kumkamata
Bwana Malimi na kumpeleka ofisi ya sungusungu na kumuweka chini ya
ulinzi ambapo mwenyekiti wa
sungusungu aliomba watoe fedha kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yao
ambapo mama huyo alitoa shilingi elfu themanini papo kwa papo huku
akimuacha hoi mmewe kwa vile alikuwa hajui fedha hizo mkewe alizitoa
wapi na hivyo alishinikiza akae rumande hadi siku inayofuata ambapo
baada ya kituo cha ITV kurusha moja kwa moja mahojiano na Katibu Mkuu wa
chama hicho ndiko kulipelekea ukombozi wa Bwana Malimi na Amewataka
wanaume kote nchini kukiunga mkono na kukiamini chama hiki kuwa ni
ukombozi wa mwanaume na ni mlinzi wa Haki za Binadamu dhidi ya ukiukwaji
wa sheria na kanuni za nchi.
Baadhi
ya wananchi wamekipongeza kituo cha ITV kwa kuwa mstari wa mbele
kuielimisha jamiin ya Watanzania nchini kwa kuita watu mbalimbali
kituoni hapo ili kuzungumzia masuala mbalimbali ambayo yana faida kwao
na wamevitaka vituo vingine viige mfano huu ili Taifa letu liendelee
kuidumisha Amani yetu kuiweka nchi katika utulivu na usalama.
Mwenyekiti wa TAMRA Bwana Belensi Alkadi akisikiliza mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu katika Hotel ya White Sands Resort jijini Dar Es Salaam |
No comments:
Post a Comment