Timu ya Taifa ZAMBIA |
TAIFA STARS |
Mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) wakiwa na msafara wa watu 32 wanatarajia kuwasili nchini kesho
(Desemba 19 mwaka huu). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Lusaka.
Mbali ya wachezaji 24, msafara wa
Zambia ambayo inakuja nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars utakuwa na
maofisa wengine wanane wakiwemo wa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha
Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Chintu
Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa,
Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac
Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo
Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani
Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Mechi dhidi ya Taifa Stars itafanyika
Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10 kamili jioni. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Kim
Poulsen kujiandaa kwa mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa
sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya
chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh.
30,000.
Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku
moja kabla ya mechi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja
wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo,
kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
Pia tiketi zitauzwa Ijumaa (Desemba 21
mwaka huu) kwenye tamasha la Kilimanjaro Premium Lager kuhamasisha washabiki wa
Taifa Stars litakalofanyika kwenye viwanja vya Sigara, Chang’ombe.
No comments:
Post a Comment