Friday, December 21, 2012
LEMA NDANI YA NYUMBA
'...nilikuwa honeymoon na sasa nimerejea...' haya ni baadhi ya maneno ya Godbless Lema baada ya hukumu yake na kumrudishia haki yake ya ubunge aliyovuliwa tarehe 05 April 2012 iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira. Kesi hiyo iliyoanzishwa na wanaCCM watatu Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel. Rufaa hiyo imesomwa Dar es Salaam leo na kuzua bonge la gumzo kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni mada ilikuwa kila mahali. Kinachosubiriwa kwa sasa ni hali itakavyokuwa mapokezi yake huku jimboni kwake arusha ambapo yeye mwenyewe kawashukuru Watanzania wote akisema hapati picha Arusha itakavyokuwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment