Thursday, December 27, 2012

ROMA KUACHIA NGOMA '2030'

Yule msanii machachali kila mahali ikiwa ni jukwaani au kusikiliza ngoma zake R.O.M.A anakuja na ngoma mpya ambayo itatoka kesho ijumaa tarehe 28 mwezi wa kumi na mbili. Jina la wimbo ikiwa ni kama kawaida yake R.O.M.A lina utata kwa mtu yeyote atakayelisikia kwa mara ya kwanza kwa sababu ni wimbo uitwao 2030............msanii huyo amesema ataelezea zaidi wimbo huo ukitoka lakini ni mwendelezo wa falsafa yake ya MATHEMATICS akisema kajaaliwa kupata mtoto mwaka huu na atakuwa mtu mzima 2030. so raia wanasubiria sana hapo kesho kuzama you tube kama mwenyewe atauweka you tube ili wausikie mashairi yake, lakini pia na uongozi wa blog hii utakupa data zaidi hapo kesho.

No comments:

Post a Comment