Sunday, December 30, 2012

ASUTA +PY MWAROBAINI KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU BAGAMOYO

ASUTA +PY MWAROBAINI KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU BAGAMOYO :

ASUTA-Asasi ya Uwezeshaji Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linasaidia jamii katika nyanza za Afya, uchumi na kiutamaduni. ASUTA iko kihalali na imesajiliwa kwa sheria za AZAKI 2002. Kwa mradi wa kuzuia maambuikizi ya VVU Bagamoyo unaofadhiliwa na RFE, ASUTA kwa ushirikiano na Progress the Youth Foundation kwa pamoja mashirika haya yameweza kufikia makundi ya watumia madawa ya kulevya, wahudumu wa bar, wafanya biashara ya ngono na wafanyakazi wa kuhamahama. 

Awali ya yote wilaya ya Bagamoyo ina kata 22 na  ina sababu nyingi kwa maambukizi ya VVU kushamiri ikiwemo ni mji wa kitalii, mji unao kaliwa na watu wa tamaduni mbalimbali toka pande zote za dunia wakiongoza kwa kuingia na kutoka. Bagamoyo au BWAGAMOYO kwa jina asili ina bandari, kuna shughuli za uvivi, usafirishaji, uingizwaji wa tamaduni ngeni tofauti na za asili unaharibu vijana na wengi kujiingiza katika tabia hatarishi kama kufanya biashara ya Ngono, kutumia madawa ya kulevya au kuuza, kuwa na wapenzi wengi n.k. Wakati mradi uanaanza maambukizi yalikuwa 9.4% takwimu za mganag mkuu wa wilaya bagamoyo pamaoja na wizara ya Afya. ASUTA imechangia sana kupunguza maambukizi ya ukimwi ambayo yamefikia takribani 7% kutokana na ripoti iliyotolewa siku ya ukimwi dunia 01/12/2012 iliyofanyika KIJIJI CHA MDAURA JIMBO LA CHALINZE. Iliratibiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kwa ushirikiano na wadau wengine ASUTA akiwa mojawapo ya washiriki wakubwa, NIHABARISHE IMEELEZWA.
NIHABARISHE imeelezwa kuwa Bagamoyo kuna AZAKI nyingi sana hizi ni habari rasmi kutoka kwenye vyanzo vya habari vya NIHABARISHE na nyingi zilishriki siku ya ukimwi duniani AZAKI hizi ni ASUTA, PROGRESS THE YOUTH FOUNDATION, BAGEA, CVM, UWAMABA, UVIWAMABA, TWISUKA, BANGONET, AWABA n.k.

Wadau wa AZAKI hizi wameomba serikali kuongeza nguvu kifedha ili kuziwesha kutekeleza shughuli ipasavyo, NIHABARISHE limeambiwa VVU bado vipo na tatizo halijaisha kutokana sababu zilizotajwa juu. Alikaliliwa mmojwapo wa wahanga wa tatizo hili aishe Kata ya DUNDA Mitaa ya mangesani akisema hili tatizo kwa wilaya yetu namuomba Mheshimiwa Rais  wa jamhuri ya muungano aingilie kati tatizo bado kubwa, bado unyapaa upo, kuambukizana kwa makusudi na lishe kwa WAVIU hakuna aksema tunakuomba Raisi wetu utupie jicho wilaya ya Bagamoyo kutukwamua kiuchumi na kiafya. NIHABARISHE lilimkalia kitako na kunyaka yaliyo yake moyo na hakusita kumwagika kama mwandishi wetu alivyotambaa nae bila kuachia singo dot ya kilichosemwa. Hivyo NIHABARISHE linaomba wadau wote akiwemo Mheshimiwa Rais DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE na wengine sio tu RFE kusaidi wilaya hii yenye changamoto lukuki jinsi ya kufikia kauli mbiu ya ukimwi duniani: 

TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAVYO NA VVU INAWEZEKANA (TANZANIA WITHOUT NEW HIV/AIDS INFECTION, ZERO DESCRIMINATION AND DEATHS RELATED TO HIV/AIODS IS POSSIBLE.
Mmoja wa maafisa wa PY alisema REACHING TO ZERO HIV/AIDS IS POSSIBLE WITH A JOINT VENTURE YES WE CAN.

Aidha kwa robo ya kwanza ya utekelezaji iliweza kuwafikia vijana 650 walioko mazingira hatarishi, vijana hawa walipatiwa elimu elimishi jinsi ya kujikinga na VVU na ukimwi. Kutokana na vyanzo habari vya NIHABARISHE imebaini kuwa vijan hawa walikuwa hawana uelewa mzuri wa kujikinga na VVU.
''Akikaliliwa kijana mmoja mfaidika wa mradi kwa jina la Stamily Idd alisema ASUTA imenisaidia kumbe kufanya apenzi bila kondom hata kama mtu unamjua si salama sasa nimejifunza nimeelewa na nitawaelimsha na wenzangu mtaa.
ASUTA imefanya mafunzo ya waelimisha rika 50 kwa siku tano mfululizo hoteli ya SYKREAD BAGAMYO. Watu walioshiriki ni wahusika wa mradi kama wahudumu wa bar, watumia madawa ya kulevya, wafanya biashara ya ngono na wafanya kazi wa kuahamahama wakiwemo wawakilishi toka kila kata wilayani Bagamoyo. Waelimisha rika hawa wataelimisha watu wengine zaidi nainakadiliwa kuwa kila mtu hueimisha zaidi ya watu 100 kwa robo ya mradi aidha ripoti ndani ya shirika baada ya nihabarishe kuchimba kwa kina na kiutafiti zaidi ilijulikana kuwa mojawapo ya waelimisha rika wameweza kufikia watu zaidi ya 1000 kwa mwezi mfano mwelimisha rika toka kata ya Msoga ambapo mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ndiyo kata ya nyumbani ameweza kufikia idadi ya watu zaidi ya 1000 kuelimisha kuhusu maambukizi ya VVU akishirikiana na mwezake Juliana.

Kwa kata ya chalinze ASUTA ina wapinaji wazuri katika kutokomeza maambukizi mapya ya VVU ambao wanatoa ripot kila robo ya utekelezaji na kila mwezi Bwana Charles Manganga na Abdallah Tiff Shabani wamesaidia sana kusambaza uelewa jinsi ya kujikinga na VVU kwa makundi ya watu walioko mazingira hatarishi.
ASUTA imenunua baiskeli na kugawa kwa waelimisha rika yaani  PHE'S, kwa mradi wa kuzuia maambukizi mapya ya VVU ROUND 9 Chini ya udhamini wa RFE na inaendelea kuwagawi kurahisha utekelezaji wa mradi. Fuatilia ripoti kamili toleo lijalo kutakuwa na vielezo na takwimu zaidi.

PICHA CHINI NI WAKATI WA MATAMASHA YA KUZUIA VVU BAGAMOYO HAPA NI CHALINZE TIMU YA MPIRA, WA KWANZA KULIA MENEJA MRADI NA MWENYE SHATI JEUSI NI DIWANI KATA YA CHALINZE

 KUZUI VVU, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAYO NA VVU NI LAZIMA MBINU NA MIKAKATI MINGI IHUSISHWE. KAULIMBIU YA MCHEZO MPIRA KWA NGONO SALAMA NA MICHEZO YOTE KWA NGONO SALAMA ILI TUFIKIE MALENGO YA MDG.
 CHINI TIMU YA MPIRA JEZI BLUE KWA JINA LA MAVAMPIRE FC VS CHALINZE VETERANI FC KUZUIA VVU BAGAMOYO NA TANZANIA KWA UJUMLA.
MABANGO YENYE UJUMBE ELIMISHI, ASUTA+PY WAMESAMBAZA MABANGO HAYA MAENEO MENGI YA BAGAMOYO KWENYE AKUTANO YA WATU KWA AJIRI YA KUZUI VVU
 VIJANA MAHIRI TOKA TOT WAKICHEZA NGOMAMUZIKI WENYE UJUMBE WA KUKINGA VVU BAGAMOYO WAKIONGOZWA NA NURDINI PAMOJA NA LETICIA KUELIMISHA NA BAADAE KUSHIRIKI UGAWAJI KONDOM NA TSHIRT ZENYE UJUMBE KUZUIA VVU 2012/08-10.
VIJANA KATIKA MAZUNGUMZO YA MASWALI NA MAJIBU KWA UHURU KWA KILA MTU KUCHANGIA FOCUS GROUP DISCUSSION & OPEN DIALOGUE.

 MAAFISA WA ASUTA WAKIWA NA WEO KATA MANDERA KWENYE UGAWAJI WA KONDOM, VIFAA ELIMISHI IKIWEMO SANAMU YA UUME, VIPEPERUSHI, KONDOM NA HUKU WAKITEKELEZA ZOEZI LA TATHIMNI M&E.
  MAAFISA WA ASUTA WA KWANZA KULIA MWENYEKITI ASUTA AKIJITOLEA KUTEKELEZA KAZI ZA MRADI AKIMKABIDHI BI MAENDELEO KATA YA LUGOBA KWENYE UGAWAJI WA KONDOM, VIFAA ELIMISHI IKIWEMO SANAMU YA UUME, VIPEPERUSHI, KONDOM NA HUKU WAKITEKELEZA ZOEZI LA TATHIMNI M&E YA MRADI 2012/06-07.
 AFISA WA ASUTA BWANA RAMADHANI SALUM  HIZA WAKATI WA UTAFITI MDOGO MWANZONI MWA MRADI SHUGHULI YA 1.2 . UTAFITI HUU ULIKUWA NA MALENGO YA KUJUA HALI HALISI YA VVU NA KUWATAMBUA WALENGWA MAPRS/WATU WALIOKO MAZINGIRA HATARISHI KWA MAJINA NA KUWAORODHESHA ILIFANYIKA KATI YA MWEZI WA 04/2012-05/2012
 BI MAENDELEO LUGOBA AKIPOKEA MABOX YA KONDOM KWA AJIRI YA WATU WA KATA YAKE KUTOKA KWA MOJAWAPO YA MAAFISA WA ASUTA MENEJA MRADI PRINCE PASTORY.

 BI MAENDELEO LUGOBA AKIPOKEA VITABU MIONGOZO YA WAELIMISHA RIKA KWA AJIRI YA WATU WA KATA YAKE NA WAELIMISHA RIKA WAKE KWA KATA YAKE ASUTA IMEFUNDISHA WAELIMISHA RIKA WAWILI.

 BI MAENDELEO LUGOBA AKIENDELEA KUPOKEA VIFAA ELIMISHI TOKA ASUTA +PY
 WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUZIA UKIMWI MSOGA WAKIPOKEA DHANA MAALUM KWA KUZUIA VVU TOKA ASUTA

 WA KWANZA KULIA MKURUNGEZI WA ASUTA AKIWA NA MWELIMISHA RIKA WA  KATA MAGOMENI MS NEZIA MANYAMA WAKIWA FIELD MAENEO YA UTENDAJI KAZI WAKIWATEMBELEA WALENGWA. AIDHA WALIWEZA KUWAFIKIA WALENGWA WENGI NA KUCHANGUA KIONGOZI WAO AMBAYE NI FARIDA ALLY RUBA AMBAYE MRADI UMEMSAIDIA AMEACHA TABIA HATARISHI, AMEELIMIKA NA ANAELIMISHA WENGINE NA AMEWEZA KUFIKIA WATU ZAIDI YA 190 WALIOKO MAZINGIRA HATARISHI NIHABARISHE ILIELEZWA. PIA FARIDA ALLY RUBA  ALIWEZA KUPATA MAFUNZO YA SIKUN TANO 2/5/2012-6/05/2012 SYKREAD HOTEL NA ALIKIRI KUWA YAMEMSAIDIA NA AMEBADIRIKA SANA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI
ASUTA
SLP 70
BAGAMOYO
Barua pepe: asutatz@gmail.com
Mob:+255754 464 393/754941134



                                                    PROGRESS THE YOUTH FOUNDATION
      Barua pepe: progresstheyouth@gmail.com
      Mob: +255712 328 862

No comments:

Post a Comment