Monday, December 31, 2012

SENSA 2012 KIKWETE AONYA

 Ongezeko la idadi ya watanzania limemstua JK,  asema watu milioni 44.9 sasa ni mzigo kwa serikali, na kuwataka Watanzania kufuata uzazi wa mpango vinginevyo hali ya maisha itakuwa tete.....
Hayo ameyasema leo katika  viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam alipokuwa akitangaza matokeo hayo ya awali ambapo pia waziri mkuu Mizengo Pinda na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Seif Ali Idd imeonesha kuwa Watanzania tupo 44,929,002. ikiwa Tanzania Bara ina idadi ya watu milioni 43,625,434 huku Zanzibar wakiwa 1,303,568.
kwa upande mwingine wadau wamesema kuwa huenda idada iko zaidi ya hapo huku wakitoa sababu kuwa kuna baadhi ya Watanzania hawakuhesabiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo na wengine kukwepa kuhesabiwa kwa sababu ya imani zao. 
                  

No comments:

Post a Comment