Wednesday, January 16, 2013

AJALI YA TRENI MISRI YAPOTEZA MAISHA YA RAIA



Treni ya jeshi nchini Misri imepata ajali na kuwauwa makuruta 17.
Msemaji wa wizara ya afya nchini humo amesema kuwa treni hiyo ilikuwa ikiwasafirisha vijana waliojiandikisha jeshini kwenda kwenye kambi ya kijeshi mjini Cairo, ilipoacha reli katika mitaa ya Giza katika eneo la Badrashin.
Watu wengine 105 walijeruhiwa katika ajali hiyo. Misri ina rekodi mbaya ya usalama wa barabara na reli. Mwezi Novemba mwaka jana treni ililigonga basi la shule lililokuwa likivuka reli mjini Cairo, na kuwauwa watu 50 wengi wao wakiwa watoto.

No comments:

Post a Comment