Friday, January 4, 2013

SIKU YA KIMATAIFA YA MAANDISHI YA BRAILLE YAADHIMISHWA DAR

Leo tarehe 4 January ndio siku ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya maandishi ya Braille na Dkt. Hussein Ali Mwinyi  waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ndiye aliyekuwa mgeni rasmi..
Maandishi ya Braille ni maandishi yatumiwayo na wasioona na yamekuwa msaada kwao sana. Siku hii imeadhimishwa na Taasisi ya Huduma na Maendeleo kwa Wasioona Tanzania (TNIB) kwa mara ya pili hapa Tanzania
Katika hotuba yake Mhe Mwinyi kalipongeza pia kanisa la Anglican Tanzania kwa kuanzisha shule ya wasioona
Pia Mh amewaomba watanzania kutunza afya za macho yao na kusisitiza kila familia wasioona wapelekwe shule huku akiahidi  wizara yake kwa kushirikiana na ile ya elimu na mafunzo ya ufundi watafanya juu  chini kuendeleza shule za wasioona na kuzipatia huduma stahiki.


No comments:

Post a Comment