Tuesday, January 22, 2013

TANZANIA YALITAKA BARAZA LA USALAMA KUENDELEZA JUHUDI ZA KUUNGA MKONO MIKAKATI YA AMANI MASHARIKI MWA KONGO


Tanzania imelitaka Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kuendelea
kuunga mkono mikakati na juhudi mbalimbali zinazolenga katika
kurejesha amani ya kudumu katika eneo laMashariki ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Wito huo umetolewa na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa Tuvako Manongi, wakati akichangia majadiliano ya wazi kuhusu
operesheni za kulinda amani na ujenzi wa amani na maendeleo.
Tuvako Manongi,

Majadaliano hayo yaliyofunguliwa na KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon, na yameandaliwa na Pakistani, nchi ambayo ni Rais wa
Baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari.
BAN KI-MOON

Katika mchango wake, Tanzania imeeleza bayana kuwa, hali iliyojitokeza
mwezi Novemba mwaka jana huko Goma, ni kielelezo na ushuhuda wa
dhahiri kwamba juhudi na mikakati mbadala ya ulinzi wa amani
inahitajika katika kuwakabili wavurugaji wa amani katika eneo hilo.
Balozi  Manongi amesisitiza kuwa ili amani ya kudumu iwepo nchini DRC,
na hususani eneo hilo la Mashariki, panahitajika pia uwepo wa vikosi
vya ulinzi wa amani vitakavyokuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi ya
haraka na wakati mwingine katika mazingira magumu kama sehemu muhimu
ya kuchagiza ufanisi na mafanikio.
Paris

No comments:

Post a Comment