Joseph Mbilinyi aka SUGU aka Mr II |
Wanasema jasiri haachi asili akiacha hana akili ni kitu ambacho kinaonekana kuendelezwa siku ya kesho na legendary wa music wa bongo fleva nchini na ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe Joseph Mbilinyi vijana wengi wakimwita mzee wa kumchana Mulugo kesho anatarajia kufanya bonge la shoo ndani ya club ya Billicanas.
Mbunge huyo mwenye historia ndefu ndani ya game la bongofleva ndani na nje ya nchi yetu TZ anatarajiwa kufanya ambacho mashabiki wake wanakitaka ambapo leo kupitia mtandao wa kijamii facebook amepost kuwapa ruhusa mashabiki wake wapange wenyewe nyimbo wanazotaka kuzisikia hapo kesho jijini Dar es Salaam kwenye hii club kongwa mjini .
Sugu anatarajiwa kupiga ngoma zake kibao ambazo zingine ni zile alipiga akiwa bado kijana anaanza muziki yaani enzi za analojia
Ikumbukwe kuwa Sugu ndiye muasisi ya movement ya VINEGA ambayo lengo kuu ni kutetea haki za wasanii Tanzania
No comments:
Post a Comment