Monday, January 14, 2013

IFM WAKINUKISHA, KOVA ATINGA NAO KIGAMBONI


Kova akipokea Malalamiko

Wanafunzi wa chuo cha usimamamizi wa Fedha IFM leo wameamua kuandamana kuelekea ofisi za wizara ya mambo ya ndani kutokana na kuchosha na tabia za wizi huko kigamboni ambako ndio wanafunzi wengi wameweka makazi
Mmoja wa wanafunzi hao amesema kuwa wameamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi kanda ya Dar es Salaam bwana Suleiman Kova kutokana na kile wanachosema vijana wake Kova wameshindwa kusimamia vyema suala la ulinzi na usalama wa watu na mali zao huko Kigamboni.
Baada ya malalamiko hayo Kova alimuru vijana hao kwenda kupanda pantoni BURE wote kuelekea kigamboni kusaka wezi hao
Kumekuwa na matukio ya vijana hao wa IFM kukabwa na kuibiwa mali zao kama Laptop na wezi ambao wamekuwa wakifanya matukio hayo kwa muda mrefu.
Chanzo cha Habari kilienda mbali zaidi na kusema kuwa wezi hao wamekuwa na Tabia chafu ya kuiba mali za wanafunzi hao na kibaya zaidi kuwabaka na wengine kuwaingilia kinyume na maumbile.
Baada ya kufika huko vijana hao wamewaona wavuvi wakasema ndio vibaka wao ndipo wakaamua kutaka kuwaamshia vagi lakini polisi walikataa kufanya kitendo hicho, polisi walipoona vijana hao hawaelewi wamekomaa kuwaamshia wenge wavuvi ndipo polisi walipoamua kukiapply kile kilichozoeleka kufanyika kwa vijana wa UDSM yaani kulipua mabomu. 


Wanachuo hao wakiingia kwenye Pantoni kuelekea Kigamboni

No comments:

Post a Comment