Saturday, January 5, 2013

WORRIORS FROM THE EAST WAJA NA NGOMA MPYA IITWAYO HAILE SELASSIE I

Ni kundi la muziki wa reggae kutoka Arusha liitwalo WORRIORS FROM THE EAST likiongozwa nae Rasta LWANDA MAGERE wameachia ngoma mpya ikiwa ni katika harakati za muziki wao. Kundi hili la muziki ni wale vibonde walichukua tuzo ya KILI MUSIC AWARD mwaka jana katika sehemu ya wimbo bora wa reggae ambapo waliingia kinyang'anyironi na wimbo wao unaotamba uitwao ARUSHA GOLD.

Hili ni moja makundi ya muziki wa reggae ambayo yamekuwa na matamasha mengi ya muziki ndani na nje ya Tanzania ambapo mwezi uliopita walikuwa nchini Kenya na siku ya mwaka mpya walihusika vyema Moshi mkoani Kilimanjaro GLACIERS BAR na ikumbukwe kuwa wametoa hii ngoma mpya ya HAILE SELASSIE I baada ya kutoka huko nchini ETHIOPIA  almaarufu kama the promised land of Africans by Jah.


BAADHI YA WASANII WA WORRIORS


No comments:

Post a Comment