|
Prof. Sospeter Muhongo |
Kinachoonekana ni kuchangiwa na mambo ya kisiasa sasa kimefikia hatua ya kumuweka njia panda mtanzania wa hali ya kawaida kiuelewa. Hii ni kutokana na sakata lla gesi kuchukua hatua mpya kila kukicha ambapo jana Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amepinga vikali kitendo kilichofanywa na wakazi wa Mtwara kuandamana kupinga gesi kupelekwa jijini Dar es Salaam. Prof Muhongo amesema kuwa vyama vya kisiasa vya upinzani vimekuwa vikitumia suala hili la gesi kusambaza habari zisizokuwa na ukweli na kusababisha wananchi kuchukua hatua zisizostahiki. Alisisiza kuwa maandamano hayo yalikuwa ya uchochezi huku baadhi ya watu wakidai maandamano yamefanywa na wakazi wa Mtwara mjini tu na huku gesi ipo huko vijijini.
No comments:
Post a Comment