Bodi ya
utendaji ya shirika la fedha la kimataifa IMF imekamilisha mapitio ya tano ya
utendaji wa uchumi wa Tanzania na mapitio ya kwanza chini ya mpango wa msaada
wa tahadhari
Akizungumza
jijini Dar es salaam Waziri wa fedha Dk.William Mgimwa amesema badi hiyo pia
imeridhia ombi la serikali ya Tanzania la kupewa msamaha wa kukiuka kigezo cha
madeni ya nje yenye masharti ya kibiashara
Waziri Mgimwa
amesema bodi hiyo pia imeridhishwa na mikakati iliyomo kwenye bajeti ya mwaka
2012/2013 ambayo amesema inazingatia uwiano mzuri baina ya matumizi ya
maendeleo na matumizi katika huduma muhimu za kijamii
Waziri huyo
amesema katika mpango huo Tanzania itanufaika na mkopo wenye masharti nafuu
toka IMF wenye thamani ya dola za Marekani milioni 114
No comments:
Post a Comment