Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia
suala la raslimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujifatufia umaarufu wa
kisiasa na kuwapotosha wananchi.
Rais
Kikwete ameyasema hayo wakati alipokutana na Balozi wa Uingereza nchini ambaye
anamaliza muda wake, Dianne Corner ambaye
alifika Ikulu, Dar Es Salaam kumuaga
Rais
Kikwete amesema kuwa ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa
kujaribu kuigawa nchi vipande vipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa
kutumia raslimali za taifa.
Balozi
Corner ambaye amekuwa Balozi wa
Uingereza nchini Tanzania kwa miaka minne amehamishiwa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC).
Wakati huo huo Rais Kikwete usiku wa leo atampokea Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (AU) na Rais wa Benin, Boni Yayi
Rais
Yayi anawasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo mara baada ya
kuwasili viongozi hao wawili watafanya mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali
yanayolihusu Bara la Afrika
No comments:
Post a Comment