Asasi ya Uwezeshaji Tanzania almaarufu kama ASUTA ikishirikiana na asasi iitwayo PROGRESS THE YOUTH FOUNDATION (PY) imeendeleza harakati zake kama ilivyo ada na siku ya juzi ijumaa na jana jumamosi imefanya matamasha makubwa katika viunga vya mji wa Bagamoyo ambapo watu Walipata muda wa kuburudika na kupata Elimu ya gonjwa hatari kwa wakubwa na wadogo UKIMWI. Asasi hiyo imejitolea kuhakikisha Tanzania bila Ukimwi inawezekana na imekuwa ikitumia njia mbalimbali kuhakikisha raia wote wanapata kuelimika juu ya UKIMWI ikiwemo kkuonesha filamu mbalimbali zenye mlengo wa kuelimisha wananchi juu ya gonjwa la UKIMWI huku ikigawa condom za aina mbalimbali bure kwa wanachi hao.
No comments:
Post a Comment