Tuesday, January 22, 2013

MAMA KIKWETE ASISITIZA SUALALA CHANJO KWA WATOTO



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amesisitiza umuhimu wa watoto wenye
umri wa chini ya miaka mitano kupewa chanjo kwa wakati, chakula chenye
virutubisho na kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwatunza ili kujenga
taifa lenye watu wenye afya bora
MAMA SALMA KIKWETE



Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) ameyasema hayo wakati akiongea na wafanyakazi wa
Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini Ufaransa ambalo licha ya kutoa
huduma mbalimbali za dharula pia linatoa huduma za afya kwa  watoto
wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Mwenyekiti huyo wa WAMA amesema kuwa ili kupunguza vifo vya watoto
wenye umri wa chini ya miaka mitano Serikali kwa kushirikiana na
shirika la GAVI kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa
chanjo ya kuzuia magonjwa ya homa ya vichomi na uti wa mgongo  nchini
Tanzania.


Mama Kikwete ameambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini
Ufaransa kwa ajili ya mwaliko wa  ziara ya kiserikali ya siku tatu.

No comments:

Post a Comment