Tasnia ya Filamu nchini imeendelea kukumbwa na majonzi ambapo leo hii msanii mwingine JUMA KILOWOKO maarufu kama SAJUKI amefariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua muda mrefu na kupelekwa India kwa matibabu. Sajuki kafariki leo alfajiri. Msanii huyu aliyezaliwa mwaka 1986 huko Songea atazikwa keshokutwa hapa hapa Dar es Salaam kwa mujibu wa maelezo ya Baba yake mzazi.
No comments:
Post a Comment